
Ashraf JK 💚💙
June 18, 2025 at 08:25 PM
Hasira husababisha mwili kuingia katika hali ya "kupigana au kukimbia," ambapo ubongo (hasa eneo la amygdala) hutuma taarifa kwenye mfumo wa fahamu unaojulikana kama “sympathetic nervous system”, na kusababisha kuzalishwa na kutolewa kwa homoni za “adrenaline na noradrenaline”. Hii huongeza mapigo ya moyo, shinikizo la damu, na kasi ya kupumua, pamoja na kukaza kwa misuli na kusababisha jasho. Damu hukimbilia kwenye misuli muhimu tu na kupungua kwenye viungo visivyo muhimu kwa wakati huo, kama mfumo wa mmeng’enyo.
Hasira pia hupunguza utendaji wa ubongo katika eneo la “prefrontal cortex”, linalohusika na maamuzi na udhibiti wa hasira, na kusababisha maamuzi ya haraka na utamkaji wa maneno machafu ya kuudhi. Kwa muda mrefu, hasira ya mara kwa mara inaweza kusababisha shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, matatizo ya usingizi, na kudhoofisha kinga ya mwili.
Kudhibiti hasira unaweza kutumia mbinu kama vile kupumua kwa kina (deep breathing), kuhesabu taratibu moja mpaka kumi au ishirini kabla ya kufanya maamuzi, kuondoka kwenye eneo husika lililopelekea hasira, au kufanya mazoezi ya kimwili kunaweza kusaidia. Kukabiliana na chanzo cha hasira kwa utulivu au kutafuta ushauri wa kitaalamu kuna faida kwa afya ya kimwili, akili, na kutunza mahusiano yako na wengine. *DHIBITI HASIRA ZAKO LEO.*
#kmt
#afyatamu
#ashrafjk
❤️
👍
2