Kigoma Region Tanzania
Kigoma Region Tanzania
June 8, 2025 at 08:15 AM
*KUADIMIKA KWA DAGAA ZIWA TANYIKA HIZI NI MOJA YA SABABU* Iko hivi, kikawaida Dagaa hushuka chini kutoka gezini kwa kufukuzwa na migebuka, migebuka hula dagaa, sasa dagaa hujinusuru kutokana na migebuka kwa kukimbilia maji ya chini kutoka gezini, hivyo na kuleta giza na ndipo wavuvi sasa huwavua dagaa kwa urahisi wanaposhuka chini. Ni toleo la kukimbizwa na migebuka na huu ndio mfumo wao wa maisha. Uvuvi haramu wa Filimayaa hufuata migebuka huko huko gezini na kuivua, tena huvua migebuka wadogo (Nyamnyam) kiasi kwamba dagaa hawashuki chini na hivyo dagaa kuanza kuadimika. Wakongomani wanapanda gezini kufuata migebuka kwa Filimayaa, Watanzania wanapanda gezini kufuata migebuka kwa Filimayaa, Warundi wanapanda gezini kufuata migebuka kwa filimayaa, Wazambia nao wanapanda gezini kufuata migebuka kwa filimayaa. Ziwa lipo katika hatari kubwa kwa ustawi wa mwambao huu. Filimayaa ni nyavu maalumu kwa kuvulia migebuka, wavu mmoja wa Filimaya unaweza kuchukua mita 70-100. Kila mtumbwi wa filimaya unakuwa na nyavu 4 na zaidi, sawa na mita 400 ukubwa wa viwanja vinne vya mipira. Eneo la Nanga kijiji cha Sibwesa peke yake kuna zaidi ya mitumbwi 500 ya Filimayaa. Uvuvi huu haramu hufanyika nyakati za usiku, wao hutupa nyavu zote kwenye maji kuanzia majira ya jioni hadi asubuhi kisha hutandua na kuchukua migebuka iliyonasa nyavuni. Kwanini samaki wa Filimayaa hawana ladha na huwahi kuharibika? ni kwasababu samaki ananasa nyavuni jioni saa mbili usiku anafia hapo anabakia anaelea kwenye maji, inapofika asubuhi ndio hutolewa na kupelekwa sokoni, kwa hivyo wanawahi kuharibika kwasababu wanakaa sana kwenye maji. Kigoma tulikuwa hatuna tabia ya kuweka samaki kwenye barafu, ila ulipokuja uvuvi huu samaki nyingi zinawekwa kwenye barafu kuepuka uharibifu mkubwa. Dagaa wamebaki wanapatikana maeneo yale yenye hifadhi za Taifa kwasababu hakuna shughuli za uvuvi ndipo dagaa hukimbilia eneo hilo la hifadhi, hifadhi ya gombe, mahale, Lake shore lodge, Nsumbu n.k Karibuni wamiliki wa vyombo vya Filimayaa tujadili swala hili kwa pamoja. https://whatsapp.com/channel/0029VabqKek7oQhlIA20XA2P
Image from Kigoma Region Tanzania: *KUADIMIKA KWA DAGAA ZIWA TANYIKA HIZI NI MOJA YA SABABU*  Iko hivi, k...

Comments