
AjiraCoach Platform
June 18, 2025 at 05:16 PM
*JINSI YA KUWASILIANA NA AJIRA PORTAL ILI UJIBIWE.*
ZIPO NJIA MBILI UNAZOWEZA KUZITUMIA:
1️⃣ KUPIGA SIMU
2️⃣ KUTUMIA EMAIL
*KUPIGA SIMU*
Hii ni njia moja wapo ambapo unaweza kuwasiliana na Ajira Portal na ukatatuliwa shida yako. Njia hii lazima uwe mvumilivu. Piga hata kwa saa nzima bila kupumzika kwa sababu namba zipo busy muda wote. Namba zenyewe ni hizi:
1. +255739160350
2. 026 216 0350
*KUTUMIA EMAIL*
Hii ni njia nzuri ya kupata majibu, lakini wengi tunakosea kutuma email. Email yako lazima iwe inaeleweka vizuri.
Mfano: Mimi shida yangu nimeweka Postgraduate Diploma wakati nina Diploma, kwa hiyo haitakubali kutuma maombi. Utaandika kama ifuatavyo:
*Subject:* KUONDOA POSTGRADUATE DIPLOMA.
*Compose:* Mimi ni AjiraCoach Platform, namba ya NIDA *2023030384666677-00002-22* email: *[email protected]* , namba ya simu: *0629157025* . Naomba kuondoa Postgraduate Diploma niliyojaza kimakosa. Mimi nina Diploma in Pharmacy, kwa hiyo nashindwa kutuma maombi.
Nina matumaini kuwa ombi langu litashughulikiwa.
👉 Utaandika kama unavyotuma maombi ya kazi kwa email.
*EMAIL ZA KUTUMIA:*
1. [email protected]
2. [email protected]
*Kama shida yako ni ya haraka, tuma email zote mbili na piga simu pia.*
*JINSI YA KUTUMIA EMAIL TAZAMA VIDEO HAPA:*
https://youtu.be/dzn1ghjfGFU?si=h_lFKYXTu4EgjnHk
*SHARE NA WENGINE*
👍
🙏
4