TheChanzo

TheChanzo

36.9K subscribers

Verified Channel
TheChanzo
TheChanzo
June 16, 2025 at 08:45 AM
*Wazazi Wahofia Matumizi ya Pedi Kusababisha Uhuni, Mabinti Watumia Magodoro Kujisitiri.* Dodoma.  Wakati jamii, wadau na serikali ikiendelea kutekeleza afua mbalimbali za hedhi salama hapa nchini, baadhi ya wasichana wanaoishi eneo la Ng’hong’hona wamekuwa wakitumia vipande vya magodoro kujisitiri wakati wa hedhi, huku sababu tamaduni na mazoea ya jamii husika yakitajwa zaidi. Utaratibu huu wa kutumia magodoro umekuwa kama sehemu ya utamaduni uliorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi, hata hivyo kufuatia kupata elimu, mabinti wengi katika eneo hilo wanatamani kuona hali hii ikibadilika katika jamii. Mwaka 2022, Martha 17, mwanafunzi wa kidato cha nne alipovunja ungo alimfuata mama yake na kumueleza hali halisi. Baada ya kumueleza alielekezwa na mama yake namna ya kutumia magodoro kujisitiri. Soma zaidi https://thechanzo.com/2025/06/13/wazazi-wahofia-matumizi-ya-pedi-kusababisha-uhuni-mabinti-watumia-magodoro-kujisitiri/
Image from TheChanzo: *Wazazi Wahofia Matumizi ya Pedi Kusababisha Uhuni, Mabinti Watumia Ma...
👍 😢 😮 3

Comments