
TheChanzo
June 17, 2025 at 06:14 AM
*Kama Tanzania Ingekuwa Timu ya Mpira Unayoshabikia, Bado Ungeipongeza Hata Kama Inakosea?*
*Na Richard Mabala*
Leo nataka kuongelea mpira na siasa. Hapana, siyo yale mapambano yasiyoisha kati ya tembo wawili ambao wanachosha majani katika ugomvi wao usioisha. Sisi tunataka kuona mpira jamani! Tunataka kufurahia mapambano uwanjani, si yale ya mezani.
Tunataka kuona ufundi wa wachezaji, si ule wa wanasheria na wengine. Tena ule wa mezani unaua, unaua hata hamu ya kuona mchezo unavyochezwa, kuuona ufundi wa wachezaji wenyewe. Tena nakumbuka wakati fulani wachezaji wa timu moja walipinga viongozi wao, wakaambiwa waondoke, hawahitaji wachezaji. Yaani, klabu ya mpira haihitaji wachezaji wa mpira! Muhimu ni viongozi, si wachezaji, lakini bila wachezaji, klabu ipo kweli? Kweli dunia iko chini juu.
Lakini nataka kuangalia kwa namna tofauti. Tuwaangalie washabiki...
Soma https://thechanzo.com/2025/06/16/kama-tanzania-ingekuwa-timu-ya-mpira-unayoshabikia-bado-ungeipongeza-hata-kama-inakosea/
