TheChanzo
June 17, 2025 at 11:04 AM
*Polisi Wazuia Mkutano wa Waandishi wa Habari wa Heche, Waeleza Sababu ni Amri ya Mahakama Iliyozuia Shuhuli za CHADEMA*
Jeshi la Polisi limeuzuia mkutano wa waandishi wa habari uliopangwa kufanyika asubuhi ya leo, Juni 17, 2025, ambapo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche alitegemewa kuzungumza.
Polisi waliofika katika eneo la mkutano walieleza kuwa, shughuli hiyo haikutakiwa kufanyika kutokana na kuwa kuna amri ya Mahakama iliyositisha shughuli zote za chama hicho.
Brenda Rupia, ambaye ni Afisa Habari wa CHADEMA, alijaribu kuelezea kuwa mkutano huo haukuwa moja kwa moja wa shughuli za chama, jambo ambalo polisi waliofika walionekana kutoridhika nalo na kusisitiza jambo la kusitisha mkutano huo ni amri.
Soma zaidi https://www.instagram.com/p/DK_4BFHtPjk/?igsh=N2xlb2o1OWVldXUx