TheChanzo

TheChanzo

36.9K subscribers

Verified Channel
TheChanzo
TheChanzo
June 19, 2025 at 09:00 AM
*Bajeti Sio Mkoba, Ni Maisha ya Kila Siku* *Na Venance Majula* Wakati nikiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pengine nilishangazwa, au kufurahishwa, na namna bajeti ya taifa ilivyowasilishwa Bungeni. Nilipenda namna Waziri wa Fedha, aliyevalia suti, akishuka kwenye ‘shangingi’ akiwa amebeba mkoba mweusi. Ilikuwa kama hafla fulani! Kamera zilimfuata na midahalo kwenye runinga iliendelea. Nilidhani ndio kilikuwa kiini cha bajeti ya taifa, yaani, ule mkoba na hotuba yenye takwimu iliyowasilishwa Bungeni kwa niaba ya Serikali. Miaka kadhaa imepita, sasa nipo kwenye nafasi ya kuyatafakari haya kwa undani zaidi. Tayari nimeshafanya kazi na vyama vya wafanyakazi, taasisi za kimataifa, na mashirika mbalimbali. Leo, ninafahamu kuwa uwasilishaji wa bajeti ya taifa sio tamasha, au hafla tena. Ni tukio muhimu mithili ya msingi wa nyumba linalobainisha hatima ya taifa letu kwa mwaka wa fedha unaofuatia... Soma https://thechanzo.com/2025/06/19/bajeti-sio-mkoba-ni-maisha-ya-kila-siku/
Image from TheChanzo: *Bajeti Sio Mkoba, Ni Maisha ya Kila Siku*    *Na Venance Majula*   Wa...
❤️ 1

Comments