
DIVINE RETREAT UPDATES AND PRAYERS
June 20, 2025 at 07:20 PM
*MASOMO YA MISA, JUNI 21 2025.*
*JUMAMOSI YA JUMA LA KUMI NA MOJA, KIPINDI CHA KAWAIDA, MWAKA C(I).*
*KUMBUKUMBU YA MTAKATIFU ALOISI GONZAGA, Mtawa.*
*RANGI YA KILITURJIA: NYEUPE🤍.*
*SOMO LA KWANZA*
Nitazidi kuusifia udhaifu wangu.
*Somo katika barua ya pili ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho (2 WAKORINTHO 12: 1 — 10)*
Ndugu: Ikitakiwa kujisifu –ijapo hakuna cha kujisifia – nitafikia maono na mafunuo aliyonijalia Bwana. Namjua mtu, mtumishi wa Kristo, aliyechukuliwa mpaka katika mbingu ya tatu zamani Za miaka kumi na minne. Lakini sijui kama alikuwako huko kwa mwili au bila mwili: Mungu anajua. Basi, namjua mtu huyo: alichukuliwa paradisini, kama mwili au bila mwili, sijui, Mungu anajua. Huko alisikia maneno yasiyosemeka, ambayo mwanadamu hana ruhusa kuyatamka. Nataka kumsifia mtu huyo, sitaki kujisifia binafsi, isipokuwa udhaifu wangu. Hakika, kama ningetaka kujisifu, nisingekuwa mjinga, maana ningesema kweli tupu. Lakini najizuia, akanijali kuliko anayoyaona na kuyasikia kwangu. Kusudi ukkubwa wa mjumbe wa Shetani, anipige makofi, nisije nikajivuna. Kwa hiyo nilimwomba Bwana mara tatu unitoke. Naye akaniambia: ufunuo usinitie majivuno, nimepatwa na mwiba mwilini, yaani Neema yangu yakutosha, maana nguvu hukomaa katika udhajfu." Basi, napenda kujisifia udhaifu wangu, ili nguvu ya Kristo ikae ndani yangu. Kwa hiyo nafurahia udhaifu, kejeli na shida, madhulumu na mahangaiko kwa ajili ya Kristo. Kwa maana ninapokuwa dhaifu ndipo ninapokuwa na nguvu.
*Neno la Bwana........*
*Tumshukuru Mungu.*
*ZABURI YA KUITIKIZANA*
Zaburi 34: 8 — 9, 10 — 11, 12 — 13 (K.) 9a
*K. Onjeni, mwone ya kuwa Bwana ni mwema.*
Malaika wa Bwana ameweka kambi kwao
kuwazunguka wale wamchao Mungu ili kuwaokoa.
Onjeni, mwone ya kuwa Bwana ni mwema.
Heri mtu yule anayetafuta hifadhi kwake. *K.*
Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake.
kwa maana wenye kumcha hawatindikiwi kitu.
Wenye nguvu hutindikiwa na wakaona njaa,
bali wanaomtafuta Bwana hawakosi chema chochote. *K.*
Njoni, enyi watoto, mnisikilize,
ili niwafundishe uchaji wa Bwana.
Ni nani mtu apendaye uzima
anayetaka kuona siku za heri? *K.*
*SHANGILIO LA INJILI*
2 Wakorintho 8: 9
*K. Aleluya. W. Aleluya.*
K Yesu Kristo, alikuwa tajiri, lakini alijifanya maskini kwa ajili yenu, ili ninyi mpate kutajirika kwa umaskini wake.
*W. Aleluya.*
*INJILI*
Msisumbukie siku ya kesho.
*† Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Mathayo (MATHAYO 6: 24 — 34)*
Wakati ule: Yesu aliwaambia wafuasi wake, "Hakuna awezaye kuwatumikia mabwana wawili: atamchukia wa kwanza na kumpenda wa pili, au atamjali wa kwanza na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na fedha. Kwa hiyo nawaambieni, msisumbukie maisha yenu kwa sababu ya kula au kunywa, wala msisumbukie miili yenu kwa sababu ya kuvaa. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndegej wa angani; hawapandi wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani, na Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si bora kuliko hao? Nani kati yenu, hata akijisumbua sana, aweza kujiongezea kimo chake dhiraa moja? Na mbona mnasumbuka kwa sababu ya mavazi? Angalieni maua ya mashambani, jinsi yameavyo: hayafanyi kazi, wala hayasokoti. Nami nawaambieni ya kuwa, hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa kama mojawapo ya hayo. Basi, kama Mungu huyavika hivi majani ya shambani yaliyopo leo na kutupwa motoni kesho, sembuse ninyi, enyi wenye imani haba? Basi, msisumbuke mkisema, Tule nini? au Tunywe nini? au Tuvae nini?' Hayo yote watu wa mataifa huyatamani. Maana Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnayahitaji. Basi, kwanza, utafuteni ufalme wa Mungu na uadilifu wake, na hayo yote mntaongezewa. Kwa hivyo, msiisumbukie siku ya kesho; kesho itajisumbukia yenyewe. Kila siku ina matatizo ya kutosha."
*Injili ya Bwana......*
*Sifa Kwako Ee Kristo.*
