
Radio Maria Tanzania
June 16, 2025 at 11:09 AM
MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA JUMATATU - 16 JUNI 2025
Mtakatifu Yohani Fransisko Regis, Padre.
Somo la Kwanza: 2Kor 6:1-10
Somo la Injili: Mathayo 5:38-42
*Msiipokee Neema ya Mungu Bure*
Ndugu wapendwa, *tunapojaliwa kitu flani mathalani pesa tunategemea kuona mabadiliko* hasa ya maendeleo ya kiroho na kimwili ingawa pia tunaweza pia kuona mabadiliko hasi katika matumizi mabaya ya kile tulichojaliwa.
1. Tumejaliwa neema na Mwenyezi Mungu kupitia Mwana wake wa pekee Yesu Kristo kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. *Tunapaswa kutenda na kuishi maisha yanayoakisi nguvu ya mageuzi ya neema hiyo.*
Nguvu ya mageuzi ya neema tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu ionekane katika maisha yetu kwa kuishi Kristo akiwa ndani yetu. *Neema itupe nguvu na uwezo wa kukataa dhambi na kutafuta utakatifu* hasa kwa kusameheana kwani tumesamehewa kwa njia ya neema yaani pasipo mastahili yetu.
2. Kukataa dhambi na kutafuta utakatifu kunajumuisha pamoja na mambo mengine, kutolipiza kisasi kama tulivyosikia katika somo la Injili yetu ya leo. *Kristo anatuhimiza ana kutuasa leo kujiepusha na kisasi.*
Barua kwa Warumi 12:17 inasema, *”msimlipe mtu yeyote uovu kwa ovu.”* Ndugu zangu tunapotumia ouvu kulipa uovu tunapingana na mafundisho ya Mungu. Tunatumia matusi kukemea matusi, tunatumia kejeli kukemea kejeli; kulipiza kisasi si jukumu letu na ndio maana tunaambiwa, *”Wapendwa, msilipize kisasi.”* Warumi 12:19.
Basi ndugu zangu, *”msiwalipe watu ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; bali watakieni baraka.”* 1Petro 3:9.
Mtakatifu Yohani Fransisko Regis, Padre; Utuombee.
Padre Ignatius Kangwele - Jimbo Katoliki Tanga
www.radiomaria.co.tz
#mariathon2025mamawamatumaini
#radiomariatzmiaka29

🙏
❤️
👍
👏
❤
😂
🥰
58