
Radio Maria Tanzania
June 17, 2025 at 04:54 AM
LEO JUNI 17, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU EMILIA WA VILAR MTAWA NA MWANZILISHI WA SHIRIKA (1856)
Emilia alikuwa mtu mwenye cheo na alitoka katika tajiri.
Alizaliwa Ufaransa ya kusini mwaka 1791 kwenye Kijiji kidogo ambako familia yake waliishi.
Alipelekwa kusoma huko Paris (Ufaransa) lakini aliitwa nyumbani alipokuwa na umri wa miaka kumi na mitano kumtunza baba yake ambaye alikuwa ni mjane wakati huo.
Baba yake almtaka aolewe lakini Emilia alikataa, mambo yalikuwa magumu sana kwa Emilia kwa sababu hakukuwepo Padre wala mtu mwingine ambaye angeweza kumshauri au kumpa mwongozo.
Katika miaka ya baadaye yeye mwenyewe alisema: "Mungu alikuwa mwongozi wangu".
Lakini hata hivyo, sivyo rahisi kutambua ni ipi sauti ya Mungu na ni ipi ya mtu mwenyewe.
Alijitolea mwenyewe kuwatunza watoto walioachwa na wazazi wao na kuwasaidia maskini waliokuwa wagonjwa.
Jambo hili lilimletea matatizo mengi hasa kwa Upande wa Baba yake ambaye alikataa isitumiwe nyumba yake kwa ajili ya wagonjwa na maskini.
Ndipo baada ya miaka kumi na mitano Emilia alirithi mali nyingi kutoka kwa babu yake mzaa mama.
Alinunua nyumba kubwa na kuanzisha kikundi cha kidini akisaidiwa na wenzake watatu na Wapostulanti kumi na wawili kwa ruhusa kutoka kwa Askofu Mkuu, wenyewe walijiita "Masista wa Mtakatifu Yosefu".
Kazi yao ilikuwa kuwatunza waliokuwa na shida hasa wagonjwa na kuwaelimisha watoto.
Licha ya kushughulikia nchi ya Ufaransa bali pia walienda katika nchi za kigeni.
Nyumba kadha zilifunguliwa huko Algeria, Tunisia, Malta, Siria, Ugiriki na Australia.
Emilia alilianzisha Shirika lake alipokuwa na umri wa miaka thelathini na minne, mwanzoni alikumbana na vipingamizi vingi.
Akaandika: "Nina majaribio mengi, lakini Mungu yupo mara kwa mara kunisaidia".
Alipata migogoro kwa sababu mambo ya fedha yalileta machafuko kutokana na makosa ya mdhamini.
Baadaye akaandika: "Nimepata fundisho, kumwamini Mungu ni bora zaidi kuliko kuangalia tu faida ya vitu".
Tangu utoto wake alisumbuliwa na na kupanda damu.
Katika miaka ya baadaye, alizidiwa na ugonjwa huu kiasi kwamba ulisababisha kifo chake mwaka 1856.
Alitangazwa Mtakatifu mwaka 1951.
MTAKATIFU EMILIA WA VILAR MTAWA NA MWANZILISHI WA SHIRIKA, UTUOMBEE.
www.radiomaria.co.tz
#mtakatifuwaleo
#mariathon2025
#radiomariatz

🙏
❤️
❤
👍
👏
😢
65