Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 17, 2025 at 06:17 AM
MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA JUMANNE - 17 JUNI 2025 Mtakatifu Emilia wa Vilar, Mtawa. Somo la Kwanza: 2Kor 8:1-9 Injili: Mathayo 5:43-48 *Ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake* Umwilisho wa Bwana wetu Yesu Kristo ni mfano kamili wa kujitoa kwa ajili ya wengine. Alizaliwa kwenye hori la wanyama (Luka 2:7), akaishi maisha ya kawaida sana mpaka anawaambia wanafunzi wake kuwa mwana wa Adam hana mahali pa kulaza kichwa chake (Mathayo 8:20), anachukuliwa kila kitu chake mpaka wanamvua nguo (Yohane 19:23), *alijifanya maskini ili sisi tunufaike, tupate ahuweni, tuwe matajiri* (Wafilipi 2:7-8). 1. Somo la kwanza linatueleza jinsi makanisa ya Makedonia (Filipi, Thesalonika na Berea; Matendo 16, 17 na 17:11) yalivyoneemeka. *Paulo anawaandikia Wakorintho juu ya neema hiyo kwa makanisa hayo ili wajifunze ukarimu* na kuwasaidia wengine. Ndugu zangu tujifunze ukarimu kama wa Makanisa haya ya Makedonia. Sio kwamba walikua matajiri au walijitosheleza, hapana, *pamoja na umaskini wao na dhiki zao walijitoa kuwasaidia wengine.* Katika zama zetu tuwe wakarimu hasa wa haki, upendo na mambo mbalimbali yanayosaidia kujengana. 2. Pamoja na ukarimu wa Makanisa ya Makedonia, *tuige ukarimu wa Kristo aliyejitoa bila kujibakiza kwa ajili yetu.* Kwa namna ya pekee tuwe wakarimu wa upendo na msamaha kama somo la Injili linavyotufundisha. Kristo Bwana wetu anatufundisha ukarimu si tu wa mambo ya kushikika kama pesa na misaada mbalimbali, bali *tuwe wakarimu wa upendo na msamaha.* Anatufundisha kuwapenda adui zetu na kuwaombea wanaotudhulumu. Hayo anayotuambia Yeye Mwenyewe aliyatenda tena katika hali ya maumivu makali sana msalabani. Kumuiga Kristo ni wito wa kila mkristo. Tujifunze kupenda na kusamehe. Basi wapendwa ndugu zangu, *“mwigeni Mungu, maana ninyi ni watoto wake wapenzi. Upendo uongoze maishe yenu* kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa sadaka.” Waefeso 5:1. Mt. Emilia wa Vilar, Mtawa; Utuombee. Padre Ignatius Kangwele - Jimbo Katoliki Tanga www.radiomaria.co.tz #maswalimaria #radiomariatzmiaka29 #mariathon2025mamawamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA JUMANNE - 17 JUNI 2025  Mtakatifu Emilia wa...
🙏 👍 ❤️ 🔥 😂 😮 50

Comments