Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 18, 2025 at 03:20 AM
LEO JUNI 18, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU YULIANA FALKONIERI BIKIRA NA MWANZILISHI WA SHIRIKA (1342) Yuliana alizaliwa katika ukoo wa Falkonieri mjini Florens (Italia). Wazazi wake walitaka kumwoza kwa kijana tajiri lakini hii haikuwa nia yake Yuliana. Alitaka kuwa Bikira, alijiunga na Utawa wa tatu wa Waserviti akaendelea kukaa nyumbani kwake kwa muda wa miaka ishirini akawa mfano kwa watu wengine kama mtu wa Sala na mwenye kufanya kitubio. Baadaye mnamo mwaka 1304, alianzisha huko Florens Shirika la Masista wa daraja la tatu wanaoitwa 'Mantelate'. Mungu alimjalia uwezo wa kuwapatanisha watu waliokwisha kosana. Alifaulu mara nyingi kuwarudisha Wakristo waliolegea katika dini yao. Aliwatunza wagonjwa kama ndugu wapendwa wa Yesu Kristo, hata wakati mwingine alivibusu vidonda vya watu hao. Shetani alimjaribu na kumsumbua mara kwa mara. Katika vishawishi hivi Yuliana alilia: "Ee Bwana wangu Yesu afadhali niteswe mateso yoyote kuliko kukuchukiza wewe kwa dhambi". Wakati wa ugonjwa wake wa mwisho, Yuliana alishindwa kumeza kitu chochote na hivi hakuweza kupokea Komunyo Takatifu. Alipatwa na sikitiko kubwa moyoni. Neno hilo liliuchoma moyo wake sana, basi alimwomba Padre amletee Hostia Takatifu apate kuiabudu. Akaletewa Sakramenti Kuu chumbani alimolala. Kisha Padre aliikaribisha Hostia hiyo kwa mgonjwa. Hostia ilichopoka yenyewe toka vidoleni mwa Padre ikatoweka, haikuonekana tena. Yuliana alitoa sauti ya furaha akisema: "Ee Yesu wangu mpole". Kisha alizima roho ilikuwa mwaka 1341. Matukio haya sio hadithi tu lakini yamethibitishwa siku kumi na nane baada ya kifo chake kwa maandiko ya Masista wanne na ya Padre aliyempelekea Hostia. Alitangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1737. MTAKATIFU YULIANA FALKONIERI BIKIRA NA MWANZILISHI WA SHIRIKA, UTUOMBEE. www.radiomaria.co.tz #mtakatifuwaleo #mariathon2025 #radiomariatz
Image from Radio Maria Tanzania: LEO JUNI 18, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU YULIANA FALKONIERI BIKI...
🙏 ❤️ 😮 26

Comments