Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 18, 2025 at 04:33 PM
UWEPO WA RADIO MARIA TANZANIA UMELETA TIJA KWA JAMII KATIKA KUWAKUZA WATU KIROHO Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Joyce Shebe wakati wa mazungumzo maalum na Viongozi wa Radio Maria Tanzania leo Juni 18, 2025 Makao Makuu ya Radio Maria Tanzania, Mikocheni Dar es Salaam. Amesema Radio Maria Tanzania mbali na kwamba ni Taasisi ya Dini, lakini bado inafanya pia maswala ya kijamii kwa kuzingatia makundi yote, ikiwa ni pamoja na Wazee, Watoto, Vijana pamoja na watu ambao wapo katika makundi maalum. Aidha, ameipongeza sana Radio Maria Tanzania kwa sala, ushauri na ushirikiano waliompatia kwa miaka yote, ambayo amekuwa kwenye uongozi Kama Mwenyekiti wa "TAMWA" na amewaahidi kuwa pamoja nao kutoa msaada pale panapohitajika. Bi. Joyce Shebe ambaye pia ni Mhariri mkuu Clouds Media, amewataka wanawake wa Radio Maria Tanzania kufanya majukumu yao kwa weledi huku wakimtanguliza Mungu mbele. "Usichukulie poa kazi yoyote utakayopewa, fanya kwa weledi na hakikisha unasimamia kile ambacho unakiona ni sawa, usiwe mtu wakuyumbishwa na usitumie nafasi yako ya mwanamke kujishushia thamani" Vile vile amewahimiza wanawake, kujitahidi kufuatilia mambo ya Teknolojia bila kujali nafasi wanazozisimamia, kwa sababu Teknolojia inakua kwa kasi. "Hakuna namna ambavyo utaachana na Teknolojia kwa zama za sasa hivi, ili usiachwe nyuma, kila mmoja akumbatie teknolojia ili ikusaidie" Amesema Bi. Joyce Shebe Pia amewataka kuzingatia kanuni msingi za uandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na kuwa na usawa wa kijinsia kwa kuzingatia makundi yote katika jamii. Amehitimisha kwa kuwaasa kuwa kila mmoja anapaswa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia usawa, ambapo amewapongeza Radio Maria kwa kuzingatia kipengele cha usawa katika ajira. Kwa upande wake Mratibu wa Radio Maria Tanzania Ndugu. Priva Lasway amempongeza Bi. Joyce Shebe kwa kuendelea kuwa chachu kwa wanawake wengine, kwa namna anavyotenda kazi mbalimbali, ambapo amesema wanawake katika utume wa Radio Maria wanafanya vizuri. Ndugu. Priva amesema kuwa kupitia sheria za usawa wa habari na maudhui Radio Maria Tanzania, inafuata sheria hiyo kwani maudhui yake yapo pande zote za dini na kijamii. Amehitimisha kwa kumshukuru Bi. Joyce Shebe kwa ushirikiano wake alioutoa katika kipindi chote cha miaka Sita (6) alichohudumu "TAMWA". Na. Tekla Revocatus Radio Maria Tanzania #radiomariatz #mahujajikatikamatumaini #mamawamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: UWEPO WA RADIO MARIA TANZANIA UMELETA TIJA KWA JAMII KATIKA KUWAKUZA W...
🙏 ❤️ 👍 💞 😢 67

Comments