
Radio Maria Tanzania
June 19, 2025 at 02:51 AM
SALA YA MALIPIZI KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU
Kadri watu wanavyozidi kuukana na kuukufuru UMungu wako, ndivyo tutakavyozidi kuabudu kwa heshima zaidi, Ee Moyo wa Mungu uliyejifanya mtu.
Kadri watu wanavyozidi kuyakataa na kayakana mafundisho yako, ndivyo tunavyozidi kuwa imara katika kuyasadiki na kuyatangaza, Ee moyo wa Mungu na mwalimu wetu
Kadri watu wanavyodharau mamlaka ya Kanisa lako, ndivyo tutakavyoyatii, Ee Moyo wa Mungu na kiongozi wetu.
Kadri watu wanavyozama katika mambo ya kidunia, ndivyo tutakavyozidi kukoleza akili zetu na roho katika injili yako, Ee Moyo wa Mungu wetu msulubiwa
Kadri watu wanavyozidi kudharau na kuzikufuru Sakramenti Takatifu, ndivyo tutakavyozidi kuziheshimu na kuzipenda, Ee moyo wa Mungu na rafiki yetu
Kadri Ibilisi anavyozidi kunyang'anya roho za watu, ndivyo tutakavyozidi kujitahidi kueneza ufalme wako, Ee moyo wa Mungu na Mfalme wetu.
Kadri unavyozidi kuchukiwa, ndivyo tutakavyozidi kukupenda, Ee Moyo wa Mungu wetu mpendwa na mpendelevu, utusaidie.
Amina.
#mahujajikatikamatumaini
#sautiyakikristonyumbanimwako
#mamawamatumaini
#mariathon2025

🙏
❤️
💞
😂
59