
Radio Maria Tanzania
June 19, 2025 at 03:17 AM
Sala ya kuomba Mchumba Mwema
Ee mwumba wetu, umewaunganisha watu katika ndoa Takatifu, nami natumaini kupokea Sakramenti hiyo na kushirikiana na mwenzangu wa ndoa maisha yangu yote.
Kwa hiyo nakuomba Ee Bwana unisaidie kuchagua kwa hekima, nipate mchumba mwema, safi na mwaminifu, nifuate zaidi uzuri wa roho kuliko wa uso, zaidi tabia njema kuliko umaridadi.
Mioyo yetu iwe ya kulingana na nia zetu zipatane, tupate kuishi pamoja na amani na kulea jamaa zetu kwa kukuheshimu wewe na baraka zako. Amina.
.
#mahujajikatikamatumaini
#sautiyakikristonyumbanimwako
#mamawamatumaini
#mariathon2025

🙏
❤️
😢
👏
🌹
107