
Radio Maria Tanzania
June 19, 2025 at 04:10 AM
LEO JUNI 19, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU ROMUALDI, ABATI (1027)
Romualdi alizaliwa Ravena (Italia) mwaka 950 hivi, hapo awali alikuwa akilikumbuka neno moja yaani kujipatia furaha katika anasa za dunia.
Lakini kilio cha moyo wake hakikumwacha kilimkaripia na kumshauri aziache hizo furaha za dunia.
Alipuuza kuisikiliza sauti hiyo kwa maana rafiki zake waovu walizidi kumshawishi.
Punde baba wa Romualdi alipigana na mmoja wa ndugu zake akamwua.
Romualdi mwenyewe alikuwa shahidi wa mapigano hayo.
Baadaye akasikia ya kwamba alikosa sana kutozuia uuaji huo akafanya kitubio kubwa kwa kosa hilo, mwisho akaingia Utawani.
Baba yake na mabwana wengine waliongoka kwa mfano wake basi walimfuata Utawani.
Romualdi alipenda sana kukaa katika upweke lakini kwa kuwa wengi waliomba ruhusa kumfuata alipaswa kujenga Monasteri nyingine.
Monasteri kubwa kupita zote ilikuwa ile ya Komaldoli kule Italia.
Na ndiyo maana Wamonaki Wabenediktini walimfuata waliitwa Wakamaldoli.
Ilitokea kwamba alishatikiwa na kijana tajiri kisa kumkaripia kwa ajili ya maisha yake ya Uasherati.
Watawa wenzake waliiamini lawama hiyo ingawa ilikuwa ya uongo.
Walimwamuru kufanya kitubio kikali wakimtazama asitolee Misa wala asikomunike.
Alibaki katika kitubio kigumu akiwa amenyamaza kwa miezi sita lakini alionywa na Mungu kuirekebisha hali ilivyokuwa kwa sababu mashtaka yalikuwa ya uongo mtupu.
Aliishi miaka sita zaidi katika nyumba hiyo ya Kitawa baada ya maonyo akiwa amenyamaa kabisa na licha ya kuwa mzee aliongeza ugumu wa maisha yake ya Kitawa badala ya kuupunguza.
Miaka ishirini kabla ya kifo chake alitabiri jinsi atakavyokufa na katika Monasteri gani na ndivyo ilivyotukia.
Alikufa peke yake katika chumba chake mwaka 1027.
Alitangazwa kuwa Mtakatifu mwaka 1595.
MTAKATIFU ROMUALDI, ABATI, UTUOMBEE.
www.radiomaria.co.tz
#mtakatifuwaleo
#mariathon2025
#radiomariatz

🙏
❤️
👍
❤
💪
52