
Radio Maria Tanzania
June 19, 2025 at 06:35 AM
TABERNAKULO NI IKULU KWA AJILI YA MFALME
Kadiri ya KKK 1379, tunaambiwa kwamba Tabernakulo (Hifadhi Takatifu) mwanzoni ilikusudiwa kutunza kwa heshima Ekaristi Takatifu kwa ajili ya kuwapelekea wagonjwa na wale wasiojiweza wasiokuwapo katika Misa.
Baada ya kuzama katika fikara ya kina ya kiimani juu ya uwepo wa Kristo katika Ekaristi Takatifu, Kanisa lilifahamu maana ya kumwabudu kimya kimya Bwana aliye chini ya maumbo ya mkate na divai, kwa sababu, iliwekwa wazi kwamba Tabernakulo lazima iwekwe mahali panapofaa, katika Kanisa ili kuwaruhusu watu kumwabudu muumba wao.
Kwa kusema hayo basi, mimi na wewe tunapaswa tutambue leo kwamba; “Tabernakulo sio mahali zinapohifadhiwa Ekaristi zilizobaki, Tabernakulo ni Ikulu kwa ajili ya mfalme.”
✍🏾 Deac Cassian Lebba DYD.
Kuelekea Sherehe ya Ekaristi Takatifu Juni 22, 2025.
.
.
#mahujajikatikamatumaini
#mamawamatumaini
#radiomariatz

🙏
❤️
👍
❤
👏
😮
71