Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 19, 2025 at 07:03 AM
MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA ALHAMIS - 19 JUNI 2025 Mtakatifu Romualdi, Abate. Somo la Kwanza: 2 Kor 11:1-11 Injili: Mathayo 6:7-15 *Naam, mchukuliane nami* Tunapoanza kusoma sura ya 11 ya waraka wa pili wa Mtume Paulo kwa Wakorintho tunakutana ombi la mwandishi kwa hadhira yake kwamba *wachukuliane naye katika mapungufu/upumbavu wake kidogo.* Tujiulize ni mapungufu yapi hayo au ni upumbavu gani? 1. Katika sehemu hii ya waraka wa pili wa Mtume Paulo kwa Wakorintho, *mwandishi ana lengo la kutetea mamlaka yake ya kitume dhidi ya upotoshaji ulioendelea.* Kuna uwezekano mkubwa kwamba waliopinga mafundisho ya Paulo waliwapotosha watu juu ya mamlaka yake ya kitume. Sura iliyotangulia yaani 10:17 Paulo ametoka kuwaambia, *“yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana”* sasa leo hii Paulo anavyotetea mamlaka yake ya kitume anaonekana kama anajisifu na hii *inaweza kuonekana ni kujichanganya kwake, ni ujinga, ni upumbavu* lakini kwa sababu ya wivu wa Kimungu alio nao kwa watu wake na uzushi uliovuma kwa kasi juu ya mamlaka yake ya kitume ilibidi Paulo ajieleze kuwa hakupungukiwa na kitu walicho nacho mitume wakuu. *Anafanya hivyo si kwa nia ya kujisifu bali kwa kuwahikikishia Wakorintho* kwamba na yeye ametumwa na Kristo kama walivyotumwa mitume wengine. 2. Ndugu wapendwa, Paulo anatufundisha *kuonesha utambulisho wetu pale inapobidi tena si kwa lengo la kujisifu na kujionesha* kuwa sisi ni wakubwa au wenye nyadhfa flani kwa manufaa binafsi bali kwa ajili ya kuwasaidia wengine. Siku hizi tunasikia semi za utambulisho ambazo zinalenga kumnufaisha mhusika na kutishia wengine. Utasikia mtu anakuuliza kwa ukali au kwa kejeli, unajua mimi ni nani? *Unanijua mimi?* Hii si sawa kabisa wapendwa. *Tusitumie vibaya utambulisho wetu.* Tusijitambulishe kwa lengo la kujinufaisha au kuogopwa na watu bali tuwasaidie. Basi ndugu zangu tuwe wanyenyekevu na kutumia nafasi zetu pale inapobidi kwa manufaa ya wengine kwani *”Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.”* Mithali 11:2. Mt. Romualdi, Abate; Utuombee. Padre Ignatius Kangwele - Jimbo Katoliki Tanga www.radiomaria.co.tz #radiomariatunatembeanapopeleoxiv #mariathon2025mamawamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA ALHAMIS - 19 JUNI 2025  Mtakatifu Romualdi,...
🙏 ❤️ 😢 40

Comments