Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 19, 2025 at 08:41 AM
TAARIFA MUHIMU KWAKO MDAU WA RADIO MARIA TANZANIA Tunayo furaha kubwa kuwatangazia kwamba Awamu ya Pili ya Vifaa kwa ajili ya vituo vipya vya Radio Maria Tanzania imeshawasili katika makao makuu yetu hapa Dar es Salaam! Katika video hii, inaonesha wakati wa kupokea na kushusha mzigo wa vifaa vya vituo vipya, ambavyo vimeagizwa kutokana na ukarimu wenu wewe mpenzi wa Radio ya Mama, kupitia kampeni zetu zilizopita. Awamu hii inatarajiwa kutimiza malengo yetu ya kuongeza vituo katika maeneo ya Tarime, Makambako, Igunga, Mafia, Inyonga na Karatu. Tunatarajia vifaa vingine awamu ya pili vitawasili katikati ya mwezi JULAI, ambavyo vitaongeza uwezo wetu wa kutoa huduma bora na kueneza ujumbe wa matumaini katika maeneo mbalimbali. Tunaendelea kuwashukuru wadau wetu wote kwa moyo wenu wa kujitolea na kwa sala zenu mnaozidi kuiombea Radio Maria Tanzania. Pamoja na Mama Bikira Maria , tunaweza kufanya mabadiliko makubwa ya Kiroho kwa kila mmoja wetu. www.radiomaria.co.tz #mahujajikatikamatumaini #sautiyakikristonyumbanimwako #mamawamatumaini #mariathon2025
🙏 ❤️ 👍 👏 😢 🧎‍♀ 66

Comments