
Radio Maria Tanzania
June 20, 2025 at 03:27 AM
LEO JUNI 20, MTAKATIFU ADALBERTI WA MAGDEBURG, ASKOFU (981)
Mtakatifu Olga binti wa Mfalme wa Urusi aliongoka kuwa Mkristo huko Konstantinopoli (Uturuki) alipokuwa na umri wa miaka sabini.
Alimwomba Mfalme Otto Mkuu wa Prusia (Ujerumani) kuwapeleka Wamisionari kuhubiri Injili huko Urusi.
Basi Mfalme Otto akapeleka kikundi kidogo chini ya uongozi wa Adalberti aliyekuwa Mtawa.
Haijulikani alikozaliwa wala wazazi wake walikuwa watu wa namna gani.
Wamisionari walipangiwa kuingia Urusi mwaka 961 lakini hawakuweza kutekeleza mpango huo kutokana na upinzani wa mtoto mpagani wa Olga.
Baadhi ya Wamisionari waliuawa lakini Adalberti alirudi Ujerumani ambapo alikuwa baadaye Mkuu wa Watawa na alijitahidi kuwasukuma Watawa wazidi kujielimisha.
Mwaka 968 alifanywa Askofu Mkuu wa Magdeburg (Ujerumani) na kwa miaka kumi na mitatu alipeleka ujumbe wa Kristo kwa wapagani wa Ulaya ya Mashariki.
Alifungua Majimbo mapya matatu akajali sana na kuhimiza nidhamu katika nyumba za Kitawa.
Alikufa mwaka 981.
MTAKATIFU ADALBERTI WA MAGDEBURG ASKOFU, UTUOMBEE.
www.radiomaria.co.tz
#mtakatifuwaleo
#mariathon2025
#radiomariatanzania

🙏
❤️
👍
🤲
43