
Radio Maria Tanzania
June 20, 2025 at 04:49 AM
AHADI 12 ZA MOYO MTAKATIFU WA YESU
Kwa wale wote watakaouheshimu Moyo wake Mtakatifu.
Bwana Yesu aliahidi.
1. Nitawajalia neema zote watakazozihitaji katika hali yao ya maisha.
2. Nitawajalia amani katika familia zao.
3. Nitawafariji katika magumu yao yote.
4. Nitakuwa kimbilio lao salama wakati wa maisha yao na zaidi sana katika saa yao ya kufa.
5. Nitawapa baraka tele katika shughuli zao zote.
6. Wakosefu watapata katika Moyo wangu chanzo na bahari ya huruma isiyo na mwisho.
7. Waamini walio vuguvugu watakuwa na bidii.
8. Waamini wenye bidii watakwea kwa upesi katika ngazi za juu za ukamilifu.
9. Nitabariki kila mahali ambapo picha au sanamu ya Moyo wangu Mtakatifu itawekwa na kuheshimiwa.
10. Nitawajalia Mapadre karama ya kuigusa mioyo migumu.
11. Wale wote watakaoeneza Ibada hii kwa wengine majina yao yataandikwa ndani ya Moyo wangu na sitawasahau kamwe.
12. Wale wote watakaopokea Sakramenti ya Ekaristi kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi kwa miezi tisa mfululizo wakiwa katika hali ya neema ya utakaso, hawatakufa wakiwa na uadui nami, nitawapa neema ya kudumu katika uaminifu hadi mwisho na hawatakufa bila kupokea Sakramenti za mwisho”.
Usifiwe Moyo Mtakatifu wa Yesu.
.
#mariathon2025
#radiomariatanzania
#mahujajikatikamatumaini

🙏
❤️
❤
👍
🤝
🥰
🩷
113