Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 20, 2025 at 05:41 AM
MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA IJUMAA - 20 JUNI 2025 Mtakatifu Adalberti wa Magdeburg, Askofu. *Moyo* Moyo katika Maandiko Matakatifu ni zaidi ya kiungo kinachosukuma damu, ni zaidi sehemu ya mihemko ya mwanadamu, *moyo ni kiini cha utu wa mtu kinachojumuisha mawazo, nia na tabia ya maadili.* 1. Mithali 4:23 inasema, *”Linda moyo wako kuliko yote utalindayo, maana ndiko zitokazo chemchemi za uzima.”* Tunafundishwa hapa umuhimu wa kulinda moyo dhidi ya athari mbaya, kwani ndio chanzo cha maisha na matendo. Ndugu zangu, tumesikia katika Injili kuwa *hazina yako iliko, ndipo utakapokuwa na moyo wako.* Tujiulize tunaweka wapi hazina zetu? Nia na madhumuni ya hekaheka za kidunia ziwe kwa ajili kuthibitisha na kuweka imara uhusiano wetu na Mwenyezi Mungu. *Tusiwe na matumizi mabaya ya kile tunachojaliwa na Mungu.* Hazina ya kweli ni kujenga uhusiano mzuri zaidi na Mungu na kutafuta Ufalme wake. Kipaombele chetu katika kutafuta mali kiwe kudumisha uhusiano na Mungu. 2. Paulo katika somo la kwanza anatufundisha jinsi ya kuweka kipaombele hicho. Ni kwa kuvumilia shida na adha mbalimbali za maisha kwa ajili ya Kristo. *Tusitafute njia za mkato,* njia za panya, kupiga madili, na kukwepa majukumu. Tumsikia jinsi Mtume Paulo alivyovumilia vifungo, vichapo, kuvamiwa na vibaka, kupigwa na mawe, kuvunjikiwa na jahazi, kukesha katika njaa, kiu, baridi bila nguo. Haya yote ni kwa ajili ya Kristo. Alikua anawekeza kwa Mungu na ndipo moyo wake ulipo. *Tuweke nia zetu katika kudumisha uhusiano na Mungu kwa kuvumilia taabu, kutotafuta njia za mkato katika maisha na kutumia rasilimali zetu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.* Basi ndugu zangu, *”kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, elekezeni mioyo yenu kwenye mambo ya juu, alikokaa Kristo,”* upande wa kulia wa Mungu. Wakolosai 3:1-2. Mtakatifu Adalberti wa Magdeburg, Askofu; Utuombee. Padre Ignatius Kangwele - Jimbo Katoliki Tanga www.radiomaria.co.tz #radiomariatanzaniamiaka20 #mariathon2025mamawamatumaini #radiomariatunatembeapamojanapapaleoxiv
Image from Radio Maria Tanzania: MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA IJUMAA - 20 JUNI 2025   Mtakatifu Adalberti...
🙏 ❤️ 26

Comments