
Radio Maria Tanzania
June 20, 2025 at 05:08 PM
NOVENA KWA HESHIMA YA MOYO SAFI WA BIKIRA MARIA
SIKU YA PILI, IJUMAA
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Amina.
SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu ninatubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye kupendeza wachukizwa na dhambi basi sitaki kukosa tena nitafanya kitubio ninaomba neema yako nipate kurudi. Amina.
TUOMBE:
Ee Bikira Maria uliye safi kabisa uliyechukuwa mimba bila dhambi, tangu mara ya kwanza kabisa, ulikuwa safi kabisa. Ee Maria mtukufu umejaa neema, wewe ni Mama wa Mungu wangu - Malkia wa Malaika na wanadamu. Ninakuheshimu kwa unyenyekevu kama Mama mteule wa Mwokozi wangu, Yesu Kristo.
Mfalme wa Amani na Bwana wa Mabwana alikuchagua kwa neema ya pekee na heshima ya kuwa Mama yake mpendwa, kwa nguvu ya Msalaba wake, alikulinda na dhambi zote, Kwa hiyo kwa nguvu na upendo wake, nina matumaini na ujasiri katika maombi yenu kwa ajili ya utakatifu na wokovu wangu.
Ninaomba kwamba maombi yako yatanileta kuiga utakatifu wako na kujisalimisha kwa Yesu na Mapenzi ya Kimungu.
Malkia wa Mbinguni, nakuomba uwe Mwokozi wangu ili unipe maombi haya...
(Taja nia yako....)
Baba yetu....X1
Salamu Maria...X1
Atukuzwe Baba...X1
Mama yangu Mtakatifu, najua kwamba ulikuwa mtiifu kwa mapenzi ya Mungu, katika kufanya ombi hili, ninajua kwamba mapenzi ya Mungu yatakuwa kamili zaidi kuliko yangu. Kwa hiyo, nijalie nipate neema ya Mungu kwa unyenyekevu kama wewe.
Kama ombi langu la mwisho, naomba uniombee niongezeke imani katika Bwana wetu mfufuka; Ninaomba uniombee niongezeke katika matumaini katika Bwana wetu mfufuka; Ninaomba uniombee niongezeke katika upendo kwa Yesu mfufuka!
Salamu Maria, umejaa Neema, Bwana yu nawe, Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Amina
#mamawamatumaini
#radiomariatz
#mahujajikatikamatumaini

🙏
❤️
❤
👍
👏
🧎♀
😂
🫂
92