Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 20, 2025 at 06:38 PM
EKARISTI NI SADAKA NA KARAMU Ekaristi Takatifu inaundwa kwa pande mbili ambazo haziwezi kutengana. Ekaristi Takatifu ni Karamu lakini pia ni Sadaka. Ndio maana mahali inapoadhimishwa ni meza lakini pia ni altare. Ni altare kwa ajili ya kutolea sadaka na meza kwa ajili ya karamu (KKK 1383). Pande hizi mbili hutegemezana na haziwezi kutengana; Ni sadaka ili iweze kuwa karamu, na pia, ni karamu kwa sababu ni sadaka. Kwa kusema hayo, Misa Takatifu ni sadaka lakini pia ni karamu kwa mara moja. Hii itufundishe pia kwamba, ukiona mahali popote iwe ni katika familia, kazini n.k. watu wanafanya karamu kubwa na kufurahi. Ujue pia kuna sadaka kubwa nyuma ya karamu hiyo. Na kinyume chake ni sawa, ukiona mahali fulani watu wanaishi bila furaha na karamu ujue sadaka imetoweka! ✍🏾 Deac Cassian Lebba DYD Kuelekea Sherehe ya Ekaristi, Rradio Maria Tanzania imekuandalia Tafakari mbalimbali. . . Picha na Daniel Lingwentu #mahujajikatikamatumaini #radiomariatz #mamawamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: EKARISTI NI SADAKA NA KARAMU  Ekaristi Takatifu inaundwa kwa pande mbi...
🙏 ❤️ 👍 👏 😉 😢 92

Comments