Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 21, 2025 at 05:11 AM
LEO JUNI 21, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU ALOISI GONZAGA MSEMINARISTI NA MTAWA (1591) Mtakatifu Aloisi Gonzaga somo wa vijana wakristo alizaliwa mwaka 1568 na wazazi wake watukufu katika jumba la Kastiglione (Italia). Alipokuwa na umri wa Miaka mitano aliingia siku moja katika Kambi ya Askari akawasikia wakisema maneno yasiyofaa naye aliyakariri maneno hayo lakini bila kujua vema nini maana yake. Katika maisha yake yote Aloisi akiendelea kuijuta dhambi hiyo ndogo kama kwamba alikiwa amekosa sana. Siku zote alikuwa na haya kwa hiyo hakutaka kutazama mwanamke usoni. Inasemekana kwamba kwa muda wa Miaka miwili alikuwa akikaa katika mji wa Malkia na wakati wote huo hakumwinulia macho hata mara moja. Kijana huyo Mtakatifu alipenda kushinda kutwa kucha mbele ya Sakramenti Takatifu ya Ekaristi kwa kulinda Roho yake safi alikuwa akisali na kufunga. Alimpenda Mama wa Mungu kwa Mapendo yasiyo mfano. Baba yake alitaka Aloisi awe Askari lakini Aloisi alitaka kuwa Mmisionari na hapo baba yake alikasirika sana. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na sita alijiunga na Shirika la Wajesuiti. Alihamia Roma (Italia) na huko akawapita wanafunzi wenzake kwa mfano bora. Mapadre wote walimsifu kwa kuwa hakuvunja Sheria hata mara moja, furaha yake ilikuwa kuwafundisha Katekisimu masikini na watu wa Shamba. Aidha alipenda kwenda kuwatazama wagonjwa hospitalini zamani zile ulitokea ugonjwa wa kuambukiza mjini Roma na Aloisi alipata ruhusa kwenda kuwatumza wagonjwa hao. Baada ya muda yeye mwenyewe aliugua ugonjwa huo mkali na kisha kupita Muda kidogo ugonjwa wake ulizidi akapokea Sakramenti ya wagonjwa, akafa mwenye kicheko cha furaha usoni mwake mwaka 1591 akiwa na umri wa miaka Ishirini na Tatu. Aliandikwa katika orodha ya Watakatifu mwaka 1726. MTAKATIFU ALOISI GONZAGA MSEMINARISTI NA MTAWA, UTUOMBEE. www.radiomaria.co.tz #mtakatifuwaleo #mariathon2025 #radiomariatz
Image from Radio Maria Tanzania: LEO JUNI 21, TUNAYAKUMBUKA MAISHA YA MTAKATIFU ALOISI GONZAGA MSEMINAR...
🙏 ❤️ 🎉 👍 😢 🥳 79

Comments