Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 21, 2025 at 09:11 AM
MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA JUMAMOSI - 21 JUNI 2025 Mtakatifu Aloyce Gonzaga, Mseminari. Somo la Kwanza: 2Kor 12:1-10 Injili: Mathayo 6:24-34. *Mwiba* Katika lugha ya Kigiriki, mwiba (skolops) au miiba iliyumika kwanza kueleza vigingi vilivyochongoka vilivyopangwa karibu na ngome ili *kutundika washambuliaji*, ilitumika pia *kulinda mashamba ya mizabibu* dhidi ya wezi, zaidi pia ilitumika *kutundika kichwa cha adui kilichokatwa na kuinuliwa kama ishara ya ushindi.* 1. Tumesikia katika somo la kwanza kwamba Paulo amepewa mwiba katika mwili. *Mwiba huu haelezi ni wa aina gani na hivyo kupelekea kuwa na tafsiri nyingi sana tofauti tofauti;* Tertulian anasema ni maumivu ya sikio, Chrysostom anasema ni maumivu ya kichwa, Agustino anasema ni adha mbalimbali Paulo alizozipata katika utumishi wake, wengine wanasema shida ya macho na kigugumizi. *Hii inaruhusu matumizi mapana ya dhana hiyo kwa aina mbalimbali za mateso au changamoyo zinazotukabili sisi waamini.* Kila mmoja wetu ana mwiba, ana changamoto flani au hali flani inayomtatiza. Mwiba huo mpendwa una dhumuni na lengo lake. *Dhumuni au lengo la mwiba huo Paulo anatuambia ni kuzuia majivuno* kutokana na ufunuo mkubwa kupita kiasi alioupata. Mwiba ni speed governor kwa Paulo. Mwiba umetumika kama njia ya kumnyenyekesha Paulo asije akajikuta anajimudu bila Mungu na hivyo kumkumbusha utegemezi wake juu ya neema na nguvu za Mungu. *Changamoto za maisha wapendwa zitukumbushe utegemezi wetu kwa Mungu* 2. *Maamuzi ya Paulo juu ya mwiba huu ni sala na unyenyekevu kwa Mungu* (2Kor 12:8). Paulo aliomba mara tatu kama Yesu alivyosali katika bustani ya Gesthemane (Marko 14:32-41). Paulo alikua mtu wa sala katika hali zote za maisha. Mungu anamtuma Malaika kumfariji Yesu na huku Paulo anapewa jibu la faraja, *”neema yangu yakutosha.”* Ndugu wapendwa, tunapokabiliana na miiba mbalimbali ya maisha tusisahau kusali, kumtegemea Mungu. *Kamwe tusitafute mbadala wa imani tu kwa sababu tunapitia changamoto mbalimbali za maisha.* Tuone changamoto hizo kama fursa za kuthibitisha na kuimarisha uhusiano wetu na Mwenyezi Mungu hasa katika sala. Hii inatupasa kuwa wanyenyekevu katika kufuata maongozi ya Roho Mtakatifu, vinginevyo tutapotea na kuangamia. Miiba ni ushindi dhidi ya adui, kiburi. Kama Paulo, tunapaswa kuona changamoto mbalimbali kama fursa za kukua kiroho. Hivyo basi, *”nyenyekeeni chini ya mkono wa enzi wa Mugu, naye atawainua kwa wakati wake, mwekeeni matatizo yenu maana Yeye anawatunzeni”* 1Petro 5:6-7. Mtakatifu Aloyce Gonzaga, Mseminari na Mtawa; Utuombee. Padre Ignatius Kangwele - Jimbo Katoliki Tanga www.radiomaria.co.tz #radiomariatanzaniamiaka20 #mahujajikatikamatumaini #mariathon2025mamawamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: MASOMO NA TAFAKARI SIKU YA JUMAMOSI - 21 JUNI 2025  Mtakatifu Aloyce G...
🙏 ❤️ 👍 🫡 24

Comments