Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

350.5K subscribers

Verified Channel
Radio Maria Tanzania
Radio Maria Tanzania
June 21, 2025 at 04:36 PM
SALA YA KILA SIKU YA KUMWEKEA YESU NAFSI YAKO Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, uliotoka damu ya kuwakomboa watu. Ee moyo asili ya mapendo makuu, tuliopendwa na mwokozi, toka Bethlehemu na Nazareti, toka juu ya msalaba, toka siku zote katika Ekaristi na hata leo bado mbinguni. Ee Moyo wa Yesu, unihurumie. Nimekuja leo na udogo wangu na dhambi zangu, nakuangukia unipokee. Moyo Mtakatifu wa mwokozi wangu leo nakupa moyo wangu mimi na kazi na mateso na Furaha nakupa yote niliyonayo Yesu wangu mwema, usinitupe. Utakase moyo wangu, uniongoze nitende matendo mema, uniokoe hatarini, unisaidie siku zote kwa neema yako, nipate kuokoka siku ya kufa, nifike salama kwako mbinguni Ee Yesu wangu, ninakuomba uwafanyizie vema jamaa zangu, pia na marafiki, wakubwa wangu na wadogo, Ninakuomba uwafanyizie wakristo wote, Ndugu zetu waamini kwa wakosefu. Ninakuomba uwafanyizie na watu wote wa nchi hii wasiokujua bado sisi sote tupone siku ya mwisho tupate kwenda kukusifu milele mbinguni Amina. . #mariathon2025 #radiomariatz #mahujajikatikamatumaini
Image from Radio Maria Tanzania: SALA YA KILA SIKU YA KUMWEKEA YESU NAFSI YAKO  Ee Moyo Mtakatifu wa Ye...
🙏 ❤️ 👍 👏 😘 😭 🧎‍♀ 85

Comments