
MKAY~TZ
May 27, 2025 at 04:24 AM
MASIKU KUMI YA DHUL-HIJJAH.🕋.
▫️kufunga siku 9 za mwanzo wa Dhul-Hijjah - pamoja na Siku ya Arafat (siku ya 9) sio lazima lakini inapendekezwa sana (mustahabb) na ina malipo makubwa. kwa sababu hizi ni katika siku zinazo pendwa zaidi na Mwenyezi Mungu
🌟Siku ya Arafa (9 Dhul-Hijjah) → Kufunga ni sunnah mu’akkadah (sunnah iliyosisitizwa sana) kwa wale wasiohiji. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kufunga kwenye siku ya Arafa kunafuta madhambi ya mwaka uliopita na mwaka ujao. (Muslim)
▫️Ikiwa uko kwenye Hajj → Hupaswi kufunga Arafa kwa sababu Mtume hakufunga akiwa amesimama Arafat. Kwa hivyo, wewe si mwenye dhambi usipofunga, lakini unakosa thawabu kubwa ikiwa unaweza kufunga - hasa siku ya Arafat.
🔷Siku 10 za kwanza za Dhul Hijjah 2025 zinatarajiwa kuanza tarehe 28 Mei jumatano 2025, kufuatia kuonekana kwa mwezi. Tarehe 9 Dhul Hijjah (Siku ya Arafah) itakuwa tarehe 5 Juni 2025 na tarehe 10 Dhul Hijjah (Eid al Adha) itakuwa tarehe 6 Juni 2025.
☘️Allah atujaalie uzima tupate kufunga sunnah hii iliyo bora 🤲
═════ ✥.❖.✥ ═════
#mkaytz #masiku 10ya Dhul hija#islam life♦️🔷

❤️
👍
2