Dyslexia Tanzania

Dyslexia Tanzania

20.1K subscribers

Verified Channel
Dyslexia Tanzania
Dyslexia Tanzania
May 26, 2025 at 11:16 AM
*KWA NINI NILIANZISHA DYSLEXIA TANZANIA NA KWA NINI USHIRIKI MBIO ZA DYSLEXIA AWARENESS* Nilihangaika kwa miaka zaidi ya 7 bila kuelewa kwa nini mwanangu alikuwa na changamoto shuleni katika vipengele vikuu vitatu vya kujifunza yaani kusoma kuandika na kuhesabu. Nilibadili walimu na kumpatia wakufunzi wa muda wa ziada bila mafanikio. Nikiwa katika shughuli zangu za utalii nilifanikiwa kukutana na mgeni kutoka taifa la marekani ambaye alinifungua macho na kunipa mwanga kwa kunitajia neno DYSLEXIA. Ufunuo huu ulibadili maisha yangu. Mwaka 2021 niliunda kikundi cha Whatsapp na kuungana na wataalam pamoja na wazazi wenye watoto wenye changamoto kama hii ili kujifunza zaidi na kupeana faraja. Kufikia mwaka 2023 niliamua kuanzisha shirika lisilo la kiserikali - Dyslexia Tanzania lenye lengo la kuongeza uelewa, kusaidia watoto na familia zinazopitia changamoto hii na kutetea elimu jumuishi. Mpaka sasa shirika hili limefanikiwa kufikia walimu zaidi ya 1000 na wazazi na walezi zaidi ya 1300 kupitia programu mbalimbali za kuelimisha jamii ikiwemo semina za kukuza uelewa mashuleni na maofisini, shule ya mtandao na matukio kama Talent Show na Dyslexia Awareness Run. *Unapoiunga mkono Dyslexia Tanzania kwa kushiriki Dyslexia Awareness Run husaidii shirika tu bali unabadilisha maisha kwa kupaza sauti kuhusu watoto wenye changamoto kama dyslexia na nyinginezo. Safari yangu ilianza na mtoto mmoja Lakini kwa msaada wako tunaweza kuwafikia maelfu na zaidi* Waweza kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii kama ifuatavyo: Website https://www.dyslexiatanzania.org/ Instagram Link https://www.instagram.com/dyslexia_tanzania/ Facebook Link https://www.facebook.com/p/Dyslexia-Tanzania-100090960036619/ Whatsapp Channel https://whatsapp.com/channel/0029VaZQZN87T8beoDO0571N Dyslexia Awareness Run https://chat.whatsapp.com/FFNxywaOW8XDqvAvBoQaOa Dyslexia Support Group link https://chat.whatsapp.com/LO6BFLBENQj4KfsBAzIoX0 Karibuni Sana!

Comments