
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
June 21, 2025 at 06:20 AM
Hakuna wakati utakaokuwa *Sahihi kabisa kwako kuanza* kamwe hakuna siku utakuwa tayari kwa kila jambo unalotamani. Ukisubiri uwe tayari, utazeeka na ndoto zako. *Mambo makubwa yanaanza na hatua ndogo zilizoimara si mambo ya kusubiri uwe na hisia nzuri za kufanya hilo jambo.*
Anza sasa hivi na kile ulicho nacho, Jenga nidhamu yako hata usipopewa motisha, Jifunze kujilazimisha hata kama hutaki, Nidhamu inakupa matokeo ambayo motisha haiwezi kukupa.
Fanya kila siku kitu kinachokusogeza karibu na wewe wa kesho unayetaka kuwa. Usisubiri mpaka usifiwe, utazamwe. Jifunze kujiamsha mwenyewe, kujiongoza mwenyewe, kujituma mwenyewe. *Watu wakiona matokeo yako, ndio watakuamini. Lakini kabla ya hapo, ni lazima ujifundishe kuamini mwenyewe.*
Kubadilika haimanishi unajaribu bahati, ni wewe kubeba majukumu. Weka mpango, jiweka wewe na malengo yako, ishi kwa kusudi. Hatima haiji kwa maombi, inakuja kwa mabadiliko ya tabia na maamuzi magumu unayokubali kuyasimamia kila siku.
Kama utaanza leo, kesho haitakuwa kama jana. Na kila siku unayoshinda ukijijenga, inakusogeza karibu na mtu unayestahili kuwa.
Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
♡ ㅤ ⎙ ⌲ 🔕
*ʳᵉᵃᶜᵗ ˢᵃᵛᵉ ˢʰᵃʳᵉ ᵘⁿᵐᵘᵗᵉ ᶜʰᵃⁿⁿᵉˡ*
👍
1