
𝗢𝗧𝗛𝗨𝗠𝗔𝗡 𝗙𝗔𝗖𝗧
June 21, 2025 at 06:52 PM
Mafanikio yako ya kesho yanategemea zaidi uwezo wako wa kutoshikamana na mafanikio yako ya leo. Ameandika Othuman Fact
Swala gumu sio ntapata nini ila nipo tayari kuacha nini ili nipate hicho ninachotamani.
Issa alikuwa na utukufu wakiUngu lakini ili apate utukufu mkubwa zaidi alilazimika kutoshikama na utukufu aliokuwa nao akawa mwanadamu kisha alipomaliza akakirimiwa utukufu na enzi kubwa zaidi.
Ulipo umeridhika ndio tatizo.
Hutaki kuachilia ulichokishika ndio maana husogei.
Tatizo sio shetani wala watu ila ni wewe uliyeendelea kubaki hapo ulipo.
Usitumie nguvu nyingi kupambana KUWA bali tumia nguvu nyingi kupambana na vitu vinavyokuzuia KUWA.
Hatupambani kuwa WATAKATIFU bali tunapambana na dhambi inayotuzuia kuwa watakatifu..
JIFUNZE...
Usipambane kuwa mkuu bali ondoka kwenye mazingira yanayokuzuia kuwa mkuu.
Usipambane kuwa mfanyabiashara mkubwa, ondoa tabia zinazokuzuia kufanikiwa kwenye ndoto yako hiyo.
Usipambane kuwa mke/mume mwema, pambana na tabia zinazokufanya usiwe bora kwa mwenzi wako.
Usipambane kuwa mtumishi, Sheikh, muhumini, mkubwa, we ondoa tu vile vikwazo vinavyokuzuia KUWA.
Usipambane kuwa bora, ondoa tu vile vinavyokukwamisha kuwa mtu bora.
Siri ni hii hapa;
ACHA KUSHIKAMANA NA VITU/WATU/TABIA/FIKRA/HADHI zinazokukwamisha.
Fanikiwa, shinda, kuwa mwema, kuwa mzuri na mwenye kuvutia, pata hekima, maarifa na ufahamu, kuwa na marafiki, kwazika, umizwa, jeruhiwa, juta, jilaumu, lala, ajiriwa, fanya biashara; ila inapokuwa swala la maisha yako jifunze KUTOSHIKAMANA na chochote kati ya hicho.
Ikibidi kubadilika, badilika, ikibidi kuacha, acha na ikibidi kuondoka, ondoka.
Follow na share kwa wengine 👉 [Othuman Fact Channel] (https://whatsapp.com/channel/0029VaLtsI46buMBVNc8Q40s)
♡ ㅤ ⎙ ⌲ 🔕
*ʳᵉᵃᶜᵗ ˢᵃᵛᵉ ˢʰᵃʳᵉ ᵘⁿᵐᵘᵗᵉ ᶜʰᵃⁿⁿᵉˡ*