NMB Bank Plc

NMB Bank Plc

276.7K subscribers

Verified Channel
NMB Bank Plc
NMB Bank Plc
June 13, 2025 at 02:44 PM
Maadhimisho ya Miaka 10 ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yamehitimishwa rasmi leo na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Peter Msofe. Uwakilishi wa Benki ya NMB umeongozwa na Bi. Josina Njambi, Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu, aliyeambatana na baadhi ya wawakilishi wa Benki na wadau mbalimbali wa maendeleo ya teknolojia. Kama Benki, tutaendelea kuwekeza katika ubunifu kwa kuifikia jamii ya vijana kupitia masuluhisho ya kidijitali, program za kukuza vipaji, na ushirikiano na taasisi za elimu, ili kuandaa kizazi cha kesho chenye uwezo wa kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa njia bunifu. #nmbkaribuyako
👍 ❤️ 🫶 😍 😮 15

Comments