
NMB Bank Plc
June 14, 2025 at 06:21 PM
📍 Pwani
Miaka mitatu mfululizo, Benki ya NMB imedhamini na kushiriki maonesho ya kimataifa ya mifugo na ufugaji bora ya Tri-Nations Livestock Expo 2025, yanayowakutanisha wadau katika mnyororo wa thamani katika sekta ya Ufugaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Katika maonesho haya, wafugaji kutoka nchi mbalimbali wameshiriki katika kuonesha mifugo yao na wamejifunza mbinu bora za ufugaji.
Maonesho haya yamefunguliwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti na uwakilishi wa Benki umeongozwa na Mkuu wetu wa Idara ya Kilimo Biashara, Nsolo Mlozi aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Bima, Martine Massawe, Meneja wetu wa Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, pamoja na wafanyakazi wengine wa Benki.
#nmbkaribuyako

👍
🥰
3