NMB Bank Plc

NMB Bank Plc

276.7K subscribers

Verified Channel
NMB Bank Plc
NMB Bank Plc
June 17, 2025 at 11:56 AM
Tumedhamini na kushiriki Kongamano la uwekezaji na kuibua fursa za kiuchumi Pemba, lililoandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na kukutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi. Kongamano hili limeongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi aliyetembelea banda letu na kuelezwa namna tulivyo mstari wa mbele kuchochea uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa bluu kupitia masuluhisho yetu bunifu. Uwakilishi wa benki umeongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Miamala, Bi. Linda Teggisa aliyeambatana na Meneja wetu wa Kanda ya Zanzibar - Bi. Naima Said Shaame pamoja na viongozi wengine wa benki. #nmbkaribuyako
Image from NMB Bank Plc: Tumedhamini na kushiriki Kongamano la uwekezaji na kuibua fursa za kiu...
👍 🙏 ❤️ 🇹🇿 6

Comments