
NMB Bank Plc
June 20, 2025 at 06:18 AM
📍Dar es Salaam
Benki ya NMB imeshiriki Tamasha la Twenzetu kwa Yesu kama mdhamini mkuu, likiwa jukwaa muhimu la kukuza mshikamano wa kiroho na kijamii hususani vijana kupitia muziki wa injili.
Kupitia tamasha hili, Benki ya NMB imedhihirisha dhamira yake ya kuunganisha jamii, teknolojia na imani katika kujenga Taifa lenye mshikamano na maendeleo.
Uwakilishi wa benki uliongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara – Filbert Mponzi, akiongozana na wafanyakazi wa Benki ya NMB.
#nmbkaribuyako

👍
🙏
❤️
👏
6