Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #aakia

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Zanzibar yapiga hatua mpya kuelekea kuanzisha Shirika la ndege la Kitaifa. Zanzibar iko katika mazungumzo na wawekezaji mbalimbali kuhusu mpango wa kuanzisha shirika lake la ndege la kitaifa hatua inayolenga kuboresha muunganiko wa visiwa hivyo na kukuza sekta ya utalii. Tangazo hilo lilitolewa Jumatatu katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichofanyika Chukwani, ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mheshimiwa Nadir Abdulatif Yussuf, alieleza kuwa serikali ya Zanzibar tayari iko katika mazungumzo na shirika la ndege la EgyptAir kuhusu mpango wa kushirikiana kuanzisha shirika hilo jipya. Mheshimiwa Yussuf alibainisha kuwa majadiliano na EgyptAir yanaendelea vizuri, na kwamba pande zote mbili tayari zimefikia makubaliano ya awali ya kuweka mfumo wa ushirikiano kwa ajili ya kuanzisha shirika la ndege la Zanzibar. Kauli hiyo imetolewa kufuatia hoja iliyotolewa na Mwakilishi wa Mtambwe, Dkt. Mohamed Ali Suleiman, ambaye aliitaka serikali kuangalia kama huu ndio wakati muafaka wa kutekeleza mpango wa muda mrefu wa kuwa na shirika la ndege litakalotambulika kitaifa kutoka Zanzibar. Ikiwa mpango huu utakamilika, utaiweka Zanzibar katika nafasi nzuri ya kushindana kikanda katika sekta ya usafiri wa anga, huku ukitarajiwa pia kuongeza idadi ya watalii wanaofika visiwani kwa urahisi zaidi. Chanzo: The Citizen #Airlines #zanzibar #newairline #aviationcareer #aakia #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKuu_o1tuFY/?igsh=bWw3ZXN5ampsMnB2 *Zanzibar yapiga hatua mpya kuelekea...

Aviation Tanzania on Instagram: "Shirika la Discover toka Ujerumani laongeza safari za moja kwa moja, Frankfurt- Zanzibar. Shirika la Ndege la @discover.airlines kutoka nchini Ujerumani limeongeza idadi ya safari za moja kwa moja katika Kisiwa cha Zanzibar, kutoka safari mbili hadi nne kwa wiki, hatua inayolenga kukidhi mahitaji ya ongezeko la watalii na wasafiri wanaowasili visiwani humo kutoka barani Ulaya. Awali, shirika Hilo lilikuwa likifanya safari zake visiwani Zanzibar kupitia Mombasa siku za Jumanne na Ijumaa. Hata hivyo, kuanzia sasa, shirika hilo limeongeza safari mbili mpya za moja kwa moja (direct flights) kutoka Frankfurt hadi Zanzibar kila Alhamis na Jumamosi, hivyo kufanya jumla ya safari nne kwa wiki. Ndege za Discover,shirika tanzu la Lufthansa Group hutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA), ambao unazidi kuimarika kama kitovu kikuu cha safari za anga Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar @zaazanzibar , uwanja huo unaongoza ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa na zaidi ya safari 62,393 kwa mwaka. #Airlines #discoverairlines #lufthansagroup #directflights #aakia #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKh67FRM3m7/?igsh=MmZ3ejZ3ZmRkaDR6 *Shirika la Discover toka Ujerumani ...

Air France yarejesha safari za moja kwa moja Kati ...

Air France yarejesha safari za moja kwa moja Kati ya Zanzibar na Ufaransa. Shirika la Ndege la Air ...

Aviation Tanzania on Instagram: "Air France yarejesha safari za moja kwa moja Kati ya Zanzibar na Ufaransa. Shirika la Ndege la Air France limeanza tena safari za moja kwa moja kati ya Ufaransa na Zanzibar, kufuatia kuwasili kwa ndege yake aina ya Boeing 787-8 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA). Ndege hiyo iliwasili siku ya jumatatu Mei 26, 2025 majira ya saa 2:57 usiku ikiwa na jumla ya abiria 125. Hii ni safari ya kwanza ya moja kwa moja kufanyika tangu mwezi Machi 2025, wakati shirika hilo lilipositisha kwa muda huduma hizo kutokana na msimu mdogo wa abiria (low season). Kwa mujibu wa ratiba mpya, Air France itakuwa ikifanya safari zake za moja kwa moja mara tatu kwa wiki yaani siku za Jumatano, Alhamisi na Jumamosi huku ikifungua fursa zaidi kwa watalii kutoka Ufaransa na mataifa jirani kutembelea visiwa vya Zanzibar. @zaazanzibar #routeexpansion #airline #airfrance #abeidamanikarumeinternationalairport #zanzibarairportauthority #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKKhjs7MIdP/?igsh=MTR3YjhhMmU0eGw0ZA== *Air France yarejesha safari za ...

Aviation Tanzania on Instagram: "Assalaam Air Kushiriki Katika Maonyesho ya Kimataifa ya ITB 2025 nchini Ujerumani. Shirika la ndege nchini Tanzania la @assalaamairtz linatarajia kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya ITB Berlin kwa mwaka 2025. Ushiriki huu unatarajiwa kukuza mtandao wa shirika hilo na kuonyesha huduma maalumu za safari za ndani ya Tanzania pamoja na maeneo bora ya utalii nchini. Maonyesho hayo yatakayofanyika kuanzia Machi 4 hadi 6, 2025 katika mji wa Berlin nchini Ujerumani yatatoa fursa kwa shirika hilo kuungana na wateja wapya na kushiriki maarifa ya tasnia ya usafiri wa anga. Maonyesho ya ITB Berlin ni hafla kubwa zaidi ya biashara katika sekta ya usafiri, ambayo hufanyika kila mwaka, huzileta pamoja kampuni mbalimbali za usafiri, ikitoa fursa ya kipekee ya kujifunza kuhusu mwenendo wa hivi karibuni katika tasnia ya usafiri, kuimarisha uhusiano na mashirika ya kibiashara, na kuwasilisha huduma na bidhaa mpya za mashirika hayo. . #aviation #aviationlovers #avgeek #aircraft #newaircraft #assalaamair #embraer190 #aakia #tcaa #tanzaniaairportsauthority #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzania✈"

https://www.instagram.com/p/DGh3wSCtmya/?igsh=cHY0YXZwZ2psNGk1 *Assalaam Air Kushiriki Katika Maony...