Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 5, 2025 at 06:59 PM
https://www.instagram.com/p/DKh67FRM3m7/?igsh=MmZ3ejZ3ZmRkaDR6 *Shirika la Discover toka Ujerumani laongeza safari za moja kwa moja, Frankfurt- Zanzibar.* Shirika la Ndege la @discover.airlines kutoka nchini Ujerumani limeongeza idadi ya safari za moja kwa moja katika Kisiwa cha Zanzibar, kutoka safari mbili hadi nne kwa wiki, hatua inayolenga kukidhi mahitaji ya ongezeko la watalii na wasafiri wanaowasili visiwani humo kutoka barani Ulaya. Awali, shirika Hilo lilikuwa likifanya safari zake visiwani Zanzibar kupitia Mombasa siku za Jumanne na Ijumaa. Hata hivyo, kuanzia sasa, shirika hilo limeongeza safari mbili mpya za moja kwa moja (direct flights) kutoka Frankfurt hadi Zanzibar kila Alhamis na Jumamosi, hivyo kufanya jumla ya safari nne kwa wiki. Ndege za Discover,shirika tanzu la Lufthansa Group hutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA), ambao unazidi kuimarika kama kitovu kikuu cha safari za anga Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar @zaazanzibar , uwanja huo unaongoza ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa na zaidi ya safari 62,393 kwa mwaka. #airlines #discoverairlines #lufthansagroup #directflights #aakia #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates

Comments