Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 27, 2025 at 04:55 PM
https://www.instagram.com/p/DKKhjs7MIdP/?igsh=MTR3YjhhMmU0eGw0ZA== *Air France yarejesha safari za moja kwa moja Kati ya Zanzibar na Ufaransa.* Shirika la Ndege la Air France limeanza tena safari za moja kwa moja kati ya Ufaransa na Zanzibar, kufuatia kuwasili kwa ndege yake aina ya Boeing 787-9 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA). Ndege hiyo iliwasili siku ya jumatatu Mei 26, 2025 majira ya saa 2:57 usiku ikiwa na jumla ya abiria 125. Hii ni safari ya kwanza ya moja kwa moja kufanyika tangu mwezi Machi 2025, wakati shirika hilo lilipositisha kwa muda huduma hizo kutokana na msimu mdogo wa abiria (low season). Kwa mujibu wa ratiba mpya, Air France itakuwa ikifanya safari zake za moja kwa moja mara tatu kwa wiki yaani siku za Jumatano, Alhamisi na Jumamosi huku ikifungua fursa zaidi kwa watalii kutoka Ufaransa na mataifa jirani kutembelea visiwa vya Zanzibar. @zaazanzibar #routeexpansion #airline #airfrance #abeidamanikarumeinternationalairport #zanzibarairportauthority #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates
❤️ 1

Comments