Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #airlinepassengers

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Kenya Airways 787-8 Dreamliner Departs JFK for Nairobi. A @officialkenyaairways 787-8 Dreamliner departed from New York’s John F. Kennedy International Airport (JFK) on its long journey to Nairobi, Kenya, on Thursday. The departure was captured live during Airline Videos Live’s broadcast from the TWA Hotel patio deck, offering viewers a striking view of the aircraft as it took off. #airline #kenyaairways #kq #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/reel/DKWYg8Rsa-G/?igsh=MXZyYXZjamExcHJ1aA== *Kenya Airways 787-8 Dreamlin...

Aviation Tanzania on Instagram: "Ukichelewa kuingia ndani ya ndege dakika 45 kabla ya safari, utazuiliwa kusafiri. Shirika la ndege la United Airlines limefanya mabadiliko katika sheria ya kuwasili kwa abiria katika ndege ambapo hivi karibuni abiria wote wanaofanya safari za ndani watatakiwa kuwasili ndani ya ndege dakika 45 kabla ya safari. Awali, sheria hiyo iliruhusu abiria kuingia ndani ya ndege dakika 30 kabla ya safari, hasa kwa wale wasio na mizigo ya inayokaguliwa (checked baggage). Lakini kuanzia Juni,3, 2025, abiria wote wa safari za ndani watahitajika kuhakikisha wamekamilisha hatua ya kuingia ndani ya ndege (check-in) angalau dakika 45 kabla ya muda wa kuondoka. United Airlines imeeleza kuwa lengo la mabadiliko haya ni kuboresha utendaji kazi wa shirika, na kuwapa wafanyakazi muda wa kutosha kuwahudumia abiria kwa mambo kama vile upangaji wa viti na mahitaji mengine muhimu kabla ya safari. Shirika hilo limeeleza kuwa abiria watakaochelewa kuingia ndani ya ndege baada ya muda uliowekwa hawataruhusiwa kusafiri. Kwa abiria wanaosafiri nje ya nchi Kwa United Airlines, sheria inawataka kuingia ndani ya ndege si chini ya dakika 60 kabla ya safari. Kwa kawaida, mashirika mengi ya ndege huwashauri abiria wa safari za ndani kufika uwanja wa ndege angalau saa mbili kabla ya muda wa kuondoka, na saa tatu kwa safari za kimataifa. Lakini, baadhi ya abiria huchelewa kwa matumaini ya kuwa na nafasi ya kuingia dakika za mwisho jambo ambalo sasa halitawezekana tena kwa safari za ndani kupitia United Airlines. #airline #unitedairlines #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKM89X9MUUv/?igsh=MWpwcnJtMnlndDdkcA== *Ukichelewa kuingia ndani ya nde...

Aviation Tanzania on Instagram: "Kenya Airways yapata Bilioni 4.6 kutokana na tiketi zilizoisha muda bila kutumiwa na abiria. Shirika la ndege la Kenya Airways limeingiza mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kutokana na tiketi ambazo hazikutumika ndani ya kipindi cha miezi 13 tangu ziliponunuliwa na abiria. Taarifa ya shirika hilo imeonesha kuwa mapato yakiyotokana na tiketi zilizopitwa na muda yameongezeka kwa asilimia 9.4 kutoka bilioni 4.2 mwaka uliopita, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kufikiwa katika kipindi cha miaka mitano. Kwa kawaida, Kenya Airways huuza tiketi mapema na huzihesabu kama madeni ya muda mfupi kwenye vitabu vyao vya fedha. Tiketi hizo hubadilika na kuwa mapato halali iwapo abiria atasafiri au atashindwa kusafiri ndani ya muda wa mwaka mmoja. Mkuu wa Idara ya Bei na Usimamizi wa Mapato katika shirika hilo, Jackson Kamande, amesema kuwa sera ya matumizi ya tiketi ya shirika hilo inalingana na viwango vya kimataifa, ambapo tiketi huwa halali kwa kipindi cha miezi 12 hadi 13 tangu zinunuliwe. Ongezeko hili la mapato limetokana na ongezeko la safari na uwekaji nafasi za tiketi kutoka kwa wateja wa shirika hilo. Chanzo-NTV Kenya #airlinerevenue #kenyaairways #kq #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKMYnRpMAcq/?igsh=OGhhb2l6emEwaWsx *Kenya Airways yapata Bilioni 4.6 ku...

Aviation Tanzania on Instagram: "Abiria atakayeinuka kabla ya ndege kusimama atatozwa faini ya Dola 70. Mamlaka ya usafiri wa anga ya Uturuki imeweka sheria mpya inayowataka abiria wote kubaki wamekaa hadi ndege itakapokuwa imesimama kikamilifu kwenye eneo la kupaki,na Kwa abiria atakayekiuka sheria hiyo atatozwa faini ya dola 70 za Kimarekani. Sheria hiyo inalenga kukomesha tabia ya abiria kuamka mapema na kuanza kupanga foleni kwenye korido mara tu ndege inapotua, kabla hata ya ndege kufika kwenye kituo cha kupaki. Mamlaka hiyo inasema hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama wa wasafiri na wafanyakazi wa ndege, na tayari mashirika ya ndege yameelekezwa kutoa maelekezo ya wazi kwa abiria kuhusu kutii agizo hilo. Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la DPA kutoka Ujerumani, mashirika ya ndege yamepewa jukumu la kuwakumbusha abiria kufunga mikanda wakati wote wa kutua hadi ndege itakapopaki, na kwamba yeyote atakayekiuka agizo hilo ataripotiwa katika mamlaka na kutozwa faini. Abiria wengi wamekuwa wakionekana wakifungua mikanda yao mara tu ndege inapotua na kuamka kuelekea mlangoni kwa lengo la kuwa wa kwanza kushuka au kuchukua mizigo yao, jambo linaloonekana kuhatarisha usalama na kuvuruga taratibu za kushuka kwa mpangilio. Turkish Airlines, shirika la taifa la Uturuki ambalo linatoa huduma ya usafiri katika nchi zaidi ya 130, tayari limeanza kutekeleza sheria hiyo. Mashirika mengine ya kimataifa kama Emirates na Qatar Airways yanaripotiwa pia kuzingatia kuanzisha utaratibu huo. #airline #turkishairlines #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKIC32nsera/?igsh=NHp6N2dlMnJmaWs3 *Abiria atakayeinuka kabla ya ndege ...