
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 28, 2025 at 03:48 PM
https://www.instagram.com/p/DKM89X9MUUv/?igsh=MWpwcnJtMnlndDdkcA==
*Ukichelewa kuingia ndani ya ndege dakika 45 kabla ya safari, utazuiliwa kusafiri.*
Shirika la ndege la United Airlines limefanya mabadiliko katika sheria ya kuwasili kwa abiria katika ndege ambapo hivi karibuni abiria wote wanaofanya safari za ndani watatakiwa kuwasili ndani ya ndege dakika 45 kabla ya safari.
Awali, sheria hiyo iliruhusu abiria kuingia ndani ya ndege dakika 30 kabla ya safari, hasa kwa wale wasio na mizigo ya inayokaguliwa (checked baggage). Lakini kuanzia Juni,3, 2025, abiria wote wa safari za ndani watahitajika kuhakikisha wamekamilisha hatua ya kuingia ndani ya ndege (check-in) angalau dakika 45 kabla ya muda wa kuondoka.
United Airlines imeeleza kuwa lengo la mabadiliko haya ni kuboresha utendaji kazi wa shirika, na kuwapa wafanyakazi muda wa kutosha kuwahudumia abiria kwa mambo kama vile upangaji wa viti na mahitaji mengine muhimu kabla ya safari.
Shirika hilo limeeleza kuwa abiria watakaochelewa kuingia ndani ya ndege baada ya muda uliowekwa hawataruhusiwa kusafiri.
Kwa abiria wanaosafiri nje ya nchi Kwa United Airlines, sheria inawataka kuingia ndani ya ndege si chini ya dakika 60 kabla ya safari.
Kwa kawaida, mashirika mengi ya ndege huwashauri abiria wa safari za ndani kufika uwanja wa ndege angalau saa mbili kabla ya muda wa kuondoka, na saa tatu kwa safari za kimataifa. Lakini, baadhi ya abiria huchelewa kwa matumaini ya kuwa na nafasi ya kuingia dakika za mwisho jambo ambalo sasa halitawezekana tena kwa safari za ndani kupitia United Airlines.
#airline #unitedairlines #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates