Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #aviataupdate

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "TCAA na Idara ya uhamiaji wasaini mpango wa kubadilishana taarifa Kidijitali. Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania @officialtcaa na Idara ya Uhamiaji @uhamiajitz leo Mei 27,2025 wameingia katika makubaliano rasmi ya kushirikiana katika kubadilishana taarifa kwa njia ya kidijitali, hatua inayolenga kuimarisha usalama wa anga, kuongeza ufanisi wa huduma, na kuboresha takwimu muhimu, hususan katika sekta ya utalii. Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dodoma katika makao makuu ya Idara ya Uhamiaji na kushuhudiwa na viongozi waandamizi kutoka taasisi zote mbili,yakisiniwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Bi. Anna Makakala. Bw. Msangi alisema kuwa mpango huu umeanzishwa katika kipindi mwafaka ambapo matumizi ya teknolojia ya kisasa yazidi kuongezeka Kwa kasi duniani. If Alieleza kuwa kupitia ushirikiano huo, TCAA itaongeza ufanisi wa operesheni zake, kuimarisha usalama wa anga na kusaidia katika udhibiti bora wa wageni wanaoingia na kutoka nchini kupitia viwanja vya ndege. Kwa upande wake, Kamishna Jenerali Makakala alibainisha kuwa Idara ya Uhamiaji itaendeleza ushirikiano wa karibu na TCAA ili kuhakikisha kuwa taarifa za abiria na safari za anga zinawasilishwa kwa usahihi na kwa wakati. Mpango huu pia unatarajiwa kuboresha ukusanyaji wa takwimu za wageni wanaoingia nchini, jambo litakalosaidia katika kupanga mikakati madhubuti ya kukuza sekta ya utalii na uchumi wa taifa kwa ujumla. #tcaa #tanzaniacivilaviationauthority #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdate"

https://www.instagram.com/p/DKKWl8mMhJF/?igsh=emt0NGtlZG1oMTZi *TCAA na Idara ya uhamiaji wasaini m...

Aviation Tanzania on Instagram: "chuo cha CATC chatunukiwa tuzo kwa Ubora Katika Mafunzo ya Usalama wa Anga. Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kimetunukiwa tuzo ya kimataifa kutokana na ubora wake katika utoaji wa mafunzo ya usalama wa anga kwa mwaka 2024, hatua inayoimarisha nafasi ya Tanzania katika ramani ya usafiri wa anga barani Afrika. Katika tathmini iliyofanywa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO), CATC imeorodheshwa miongoni mwa taasisi tatu bora katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAF), na imeingia kwenye orodha ya taasisi tisa bora za mafunzo ya anga barani Afrika kwa ujumla. Tuzo hiyo iliwasilishwa rasmi tarehe 19 Mei 2025 katika hafla maalum iliyofanyika makao makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekta ya anga akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, alimkabidhi tuzo hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA, Dkt. Hamis Mwinyimvua, kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa chuo cha CATC katika kukuza usalama wa anga kupitia mafunzo bora na yenye viwango vya kimataifa. #catc #aviationtraining #aviationlovers #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdate"

https://www.instagram.com/p/DJ3ykGPsn2N/?igsh=MWhhb2syamUxMXp5dg== *Chuo cha CATC chatunukiwa tuzo ...