
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 20, 2025 at 10:31 AM
https://www.instagram.com/p/DJ3ykGPsn2N/?igsh=MWhhb2syamUxMXp5dg==
*Chuo cha CATC chatunukiwa tuzo kwa Ubora Katika Mafunzo ya Usalama wa Anga*
Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kimetunukiwa tuzo ya kimataifa kutokana na ubora wake katika utoaji wa mafunzo ya usalama wa anga kwa mwaka 2024, hatua inayoimarisha nafasi ya Tanzania katika ramani ya usafiri wa anga barani Afrika.
Katika tathmini iliyofanywa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO), CATC imeorodheshwa miongoni mwa taasisi tatu bora katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAF), na imeingia kwenye orodha ya taasisi tisa bora za mafunzo ya anga barani Afrika kwa ujumla.
Tuzo hiyo iliwasilishwa rasmi tarehe 19 Mei 2025 katika hafla maalum iliyofanyika makao makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekta ya anga akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, alimkabidhi tuzo hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA, Dkt. Hamis Mwinyimvua, kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa chuo cha CATC katika kukuza usalama wa anga kupitia mafunzo bora na yenye viwango vya kimataifa.
#catc #aviationtraining #aviationlovers #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdate