Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 27, 2025 at 03:21 PM
https://www.instagram.com/p/DKKWl8mMhJF/?igsh=emt0NGtlZG1oMTZi *TCAA na Idara ya uhamiaji wasaini mpango wa kubadilishana taarifa Kidijitali.* Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania @officialtcaa na Idara ya Uhamiaji @uhamiajitz leo Mei 27,2025 wameingia katika makubaliano rasmi ya kushirikiana katika kubadilishana taarifa kwa njia ya kidijitali, hatua inayolenga kuimarisha usalama wa anga, kuongeza ufanisi wa huduma, na kuboresha takwimu muhimu, hususan katika sekta ya utalii. Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dodoma katika makao makuu ya Idara ya Uhamiaji na kushuhudiwa na viongozi waandamizi kutoka taasisi zote mbili,yakisiniwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Bi. Anna Makakala. Bw. Msangi alisema kuwa mpango huu umeanzishwa katika kipindi mwafaka ambapo matumizi ya teknolojia ya kisasa yazidi kuongezeka Kwa kasi duniani. If Alieleza kuwa kupitia ushirikiano huo, TCAA itaongeza ufanisi wa operesheni zake, kuimarisha usalama wa anga na kusaidia katika udhibiti bora wa wageni wanaoingia na kutoka nchini kupitia viwanja vya ndege. Kwa upande wake, Kamishna Jenerali Makakala alibainisha kuwa Idara ya Uhamiaji itaendeleza ushirikiano wa karibu na TCAA ili kuhakikisha kuwa taarifa za abiria na safari za anga zinawasilishwa kwa usahihi na kwa wakati. Mpango huu pia unatarajiwa kuboresha ukusanyaji wa takwimu za wageni wanaoingia nchini, jambo litakalosaidia katika kupanga mikakati madhubuti ya kukuza sekta ya utalii na uchumi wa taifa kwa ujumla. #tcaa #tanzaniacivilaviationauthority #aviationcareer #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdate

Comments