Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #aviationtraining

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Wanafunzi wa Shule ya Alpha wapelekwa Kenya kupata mafunzo ya urubani wakati wa likizo. Shule ya Sekondari ya @alphaschoolstz imewapeleka wanafunzi wake nchini Kenya kwa ajili ya kupata mafunzo ya urubani katika kipindi cha likizo ya mwezi wa sita. Hii ni sehemu ya mwendelezo wa somo la Aviation lililoanzishwa na shule hiyo mwezi Mei 2022 kwa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza hadi cha Sita. Kupitia programu hii ya kipekee, wanafunzi hujifunza kwa vitendo urushaji wa ndege pamoja na kupata uzoefu na ujuzi wa kutosha katika sekta ya usafiri wa anga. Mafunzo haya yanajumuisha vipindi vya nadharia darasani pamoja na mazoezi ya kurusha ndege yanayofanyika moja kwa moja kwa vitendo. Programu hii inalenga kuwajengea wanafunzi msingi bora wa taaluma ya urubani na kuwaandaa kwa fursa mbalimbali ndani ya sekta ya anga, huku wakiendelea kufuata ndoto zao za kuwa marubani wa baadaye. #aviationtraining #alphaschool #futureaviators #aviationcareer #futurepilots #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DK1r4EfNtRu/?igsh=bzQwbGUwM2R6a2l1 *Wanafunzi wa Shule ya Alpha wapelek...

Aviation Tanzania on Instagram: "chuo cha CATC chatunukiwa tuzo kwa Ubora Katika Mafunzo ya Usalama wa Anga. Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kimetunukiwa tuzo ya kimataifa kutokana na ubora wake katika utoaji wa mafunzo ya usalama wa anga kwa mwaka 2024, hatua inayoimarisha nafasi ya Tanzania katika ramani ya usafiri wa anga barani Afrika. Katika tathmini iliyofanywa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO), CATC imeorodheshwa miongoni mwa taasisi tatu bora katika kanda ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAF), na imeingia kwenye orodha ya taasisi tisa bora za mafunzo ya anga barani Afrika kwa ujumla. Tuzo hiyo iliwasilishwa rasmi tarehe 19 Mei 2025 katika hafla maalum iliyofanyika makao makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekta ya anga akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, alimkabidhi tuzo hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA, Dkt. Hamis Mwinyimvua, kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa chuo cha CATC katika kukuza usalama wa anga kupitia mafunzo bora na yenye viwango vya kimataifa. #catc #aviationtraining #aviationlovers #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdate"

https://www.instagram.com/p/DJ3ykGPsn2N/?igsh=MWhhb2syamUxMXp5dg== *Chuo cha CATC chatunukiwa tuzo ...

Aviation Tanzania on Instagram: "Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kinatarajia kuanza awamu mpya ya mafunzo ya urushaji wa ndege nyuki (drones) kuanzia April, 8, 2025. Mafunzo haya yanalenga kuwapa washiriki ujuzi wa kitaalamu katika uendeshaji wa ndege zisizo na rubani, ambazo zinazidi kutumika katika sekta mbalimbali kama sekta ya usalama, kilimo, utafiti na usafirishaji wa mizigo midogo. Kwa mujibu wa CATC, mafunzo haya yatadumu kwa muda wa wiki nne na gharama ya ada ni Shilingi milioni 1.4 za Kitanzania. Mbali na gharama za ada, mshiriki atatakiwa kulipia gharama za vipimo vya kiafya ambavyo atatakiwa kuvifanya kabla ya kuanza mafunzo. Mafunzo haya yanatarajiwa kusaidia kuongeza idadi ya marubani wa ndege nyuki waliobobea, kuendana na maendeleo ya teknolojia ya anga nchini Tanzania. #aviationtraining #dronepilot #catctanzania #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv"

https://www.instagram.com/p/DGXRyhftJbJ/?igsh=c2p4b280a3gyYngw *Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Ang...