Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #dronepilot
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Tazama jinsi “drones”zinavyotumika kupulizia dawa za kuua wadudu shambani Wilayani Igunga. Mbali na matumizi ya kawaida ya ndege nyuki (drones) kwa ajili ya kurekodi picha na video katika uzalishaji wa maudhui, teknolojia hii pia inatumika kwa matumizi mengine muhimu. Katika Wilaya ya Igunga, ndege nyuki (drones) zinatumika katika shughuli za kilimo hasa katika zoezi la kumwaga dawa za wadudu hatari kwa mazao. Drone hizi zimetajwa kurahisisha zoezi la umwagiliaji wa dawa, ambapo inatumia dakika sita kumwagilia shamba la hekari moja, tofauti na awali ambapo wakulima walitumia muda mrefu zaidi kukamilisha zoezi hilo huku wakikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo wadudu kuhamia eneo ambalo halijapuliziwa dawa. Zoezi hili la kupulizia dawa ya wadudu mashambani sehemu ya mradi wa Build a better Tomorrow (BBT) uliochini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Video credit @gersonmsigwa #drone #dronepilot #aviationinagriculture #bbt #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DKO3_5SMbyV/?igsh=cWx0NjRwd3NhdWl0 *Tazama jinsi “drones”zinavyotumi...
Aviation Tanzania on Instagram: "Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kinatarajia kuanza awamu mpya ya mafunzo ya urushaji wa ndege nyuki (drones) kuanzia April, 8, 2025. Mafunzo haya yanalenga kuwapa washiriki ujuzi wa kitaalamu katika uendeshaji wa ndege zisizo na rubani, ambazo zinazidi kutumika katika sekta mbalimbali kama sekta ya usalama, kilimo, utafiti na usafirishaji wa mizigo midogo. Kwa mujibu wa CATC, mafunzo haya yatadumu kwa muda wa wiki nne na gharama ya ada ni Shilingi milioni 1.4 za Kitanzania. Mbali na gharama za ada, mshiriki atatakiwa kulipia gharama za vipimo vya kiafya ambavyo atatakiwa kuvifanya kabla ya kuanza mafunzo. Mafunzo haya yanatarajiwa kusaidia kuongeza idadi ya marubani wa ndege nyuki waliobobea, kuendana na maendeleo ya teknolojia ya anga nchini Tanzania. #aviationtraining #dronepilot #catctanzania #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv"
https://www.instagram.com/p/DGXRyhftJbJ/?igsh=c2p4b280a3gyYngw *Chuo cha Mafunzo ya Usafiri wa Ang...
Aviation Tanzania on Instagram: "Mbali na matumizi ya kawaida ya ndege nyuki (drones) kwa ajili ya kurekodi picha na video katika uzalishaji wa maudhui, teknolojia hii pia inatumika kwa matumizi mengine muhimu. Katika Wilaya ya Korogwe, drones zinatumika kufukuza wanyama wakubwa kama tembo ili kuzuia wasiingie katika makazi ya watu wanaoishi jirani na hifadhi ya wanyamapori. 🎥 credit- @kadoshitv_ . #drone #dronepilot #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviationcareer #aviationtanzania✈ #aviata #aviataupdates #aviatamedia #aviatatv"
https://www.instagram.com/reel/DGORg9TNmxV/?igsh=MTMzZnp4bmRvdjJrcA== Mbali na matumizi ya kawaida ...