Find WhatsApp Channels
Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.
Channels & Posts for #londonheathrowairport
Posts
Aviation Tanzania on Instagram: "Shehena ya simu 1000 zilizoibiwa yakamatwa uwanja wa ndege zikipelekwa Afrika kaskazini. Polisi nchini Uingereza wamekamata shehena ya simu 1,000 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow, ikiwa ni sehemu ya oparesheni kubwa dhidi ya mitandao ya kihalifu inayojihusisha na wizi wa simu jijini London. Taarifa hiyo ilitolewa na Jeshi la Polisi la Jiji la London (Met Police) juni 3 mwaka huu, wakati wa kutoa ushahidi mbele ya Bunge la Uingereza kuhusu ongezeko la wizi wa simu katika mji huo mkuu, ambapo takribani simu 80,000 ziliripotiwa kuibwa katika mwaka 2024 pekee. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Teknolojia na Takwimu za Kidijitali wa Met, Darren Scates, takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 75 ya simu zinazoporwa huishia kupelekwa nje ya nchi, huku asilimia kubwa kati ya hizo zikipelekwa nchini Algeria na China/Hong Kong. Alifafanua kuwa Algeria na China kwa sasa ndio maeneo yanayopokea kwa kiwango kikubwa simu hizo. Alieleza kuwa miongoni mwa mafanikio ya hivi karibuni ni kukamatwa kwa zaidi ya simu 1,000 zilizoibwa katika Uwanja wa Heathrow, ambazo zilikuwa zikielekea Afrika Kaskazini. Hata hivyo, polisi hawakutaja tarehe halisi ya tukio hilo, wakieleza kuwa limefanyika miezi kadhaa iliyopita na uchunguzi bado unaendelea. Scates alisema kuwa utafiti uliofanywa unaonesha kuwa asilimia 80 ya simu zilizoibwa ni aina ya iPhone, na kila moja huwa na thamani ya mtaani ya kati ya paundi 300 hadi 400 Kwa ujumla, thamani ya simu zote zilizoibwa inakadiriwa kufikia paundi milioni 20. #airport #londonheathrowairport #airportinvestigation #northafrica #smartphones #aviationupdate #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzanianews"
https://www.instagram.com/p/DK6ZyrXtyoO/?igsh=MXA2aXVhcGwxYmU3MA== *Shehena ya simu 1000 zilizoibiw...
Aviation Tanzania on Instagram: "Polisi wamdhibiti mwanaume aliyekuwa anakimbia katikati ya uwanja wa ndege wa Heathrow. Katika hali isiyo ya kawaida, mwanaume mmoja alizua taharuki kwa muda mfupi baada ya kuonekana akikimbia kwenye njia ya ndege (taxiway) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow mjini London. Tukio hilo lilitokea Juni 10 2025, na lilinaswa katika video na kituo maarufu cha Big Jet TV. Mwanamume huyo alionekana akiwa karibu na ndege ya shirika la Air Baltic kabla ya kuanza kukimbia kwenye njia ya ndege huku gari la uwanja wa ndege likimfuatilia. Wafanyakazi wa uwanja huo waliovaa mavazi ya usalama walimkimbiza na kufanikiwa kumkamata. Dakika chache baadaye, gari la Polisi wa Metropolitan liliwasili na kumchukua mtu huyo. Msemaji wa Uwanja wa Ndege wa Heathrow alithibitisha kuwa tukio hilo lilidhibitiwa haraka kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, na hakukuwa na ucheleweshaji wa safari wala athari kwa wasafiri. #airport #londonheathrowairport #taxiway #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"
https://www.instagram.com/reel/DKtcCDXNSYR/?igsh=MXgzZXZuYW1ybWVjMw== *Polisi wamdhibiti mwaume ali...