
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 10, 2025 at 06:29 AM
https://www.instagram.com/reel/DKtcCDXNSYR/?igsh=MXgzZXZuYW1ybWVjMw==
*Polisi wamdhibiti mwaume aliyekuwa anakimbia katikati ya uwanja wa ndege wa Heathrow.*
Katika hali isiyo ya kawaida, mwanaume mmoja alizua taharuki kwa muda mfupi baada ya kuonekana akikimbia kwenye njia ya ndege (taxiway) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow mjini London.
Tukio hilo lilitokea Juni 10 2025, na lilinaswa katika video na kituo maarufu cha Big Jet TV. Mwanamume huyo alionekana akiwa karibu na ndege ya shirika la Air Baltic kabla ya kuanza kukimbia kwenye njia ya ndege huku gari la uwanja wa ndege likimfuatilia.
Wafanyakazi wa uwanja huo waliovaa mavazi ya usalama walimkimbiza na kufanikiwa kumkamata. Dakika chache baadaye, gari la Polisi wa Metropolitan liliwasili na kumchukua mtu huyo.
Msemaji wa Uwanja wa Ndege wa Heathrow alithibitisha kuwa tukio hilo lilidhibitiwa haraka kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, na hakukuwa na ucheleweshaji wa safari wala athari kwa wasafiri.
#airport #londonheathrowairport #taxiway #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates