
Aviation Tanzania 🇹🇿
June 15, 2025 at 07:10 AM
https://www.instagram.com/p/DK6ZyrXtyoO/?igsh=MXA2aXVhcGwxYmU3MA==
*Shehena ya simu 1000 zilizoibiwa yakamatwa uwanja wa ndege zikipelekwa Afrika kaskazini*
Polisi nchini Uingereza wamekamata shehena ya simu 1,000 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow, ikiwa ni sehemu ya oparesheni kubwa dhidi ya mitandao ya kihalifu inayojihusisha na wizi wa simu jijini London.
Taarifa hiyo ilitolewa na Jeshi la Polisi la Jiji la London (Met Police) juni 3 mwaka huu, wakati wa kutoa ushahidi mbele ya Bunge la Uingereza kuhusu ongezeko la wizi wa simu katika mji huo mkuu, ambapo takribani simu 80,000 ziliripotiwa kuibwa katika mwaka 2024 pekee.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Teknolojia na Takwimu za Kidijitali wa Met, Darren Scates, takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 75 ya simu zinazoporwa huishia kupelekwa nje ya nchi, huku asilimia kubwa kati ya hizo zikipelekwa nchini Algeria na China/Hong Kong. Alifafanua kuwa Algeria na China kwa sasa ndio maeneo yanayopokea kwa kiwango kikubwa simu hizo.
Alieleza kuwa miongoni mwa mafanikio ya hivi karibuni ni kukamatwa kwa zaidi ya simu 1,000 zilizoibwa katika Uwanja wa Heathrow, ambazo zilikuwa zikielekea Afrika Kaskazini.
Hata hivyo, polisi hawakutaja tarehe halisi ya tukio hilo, wakieleza kuwa limefanyika miezi kadhaa iliyopita na uchunguzi bado unaendelea.
Scates alisema kuwa utafiti uliofanywa unaonesha kuwa asilimia 80 ya simu zilizoibwa ni aina ya iPhone, na kila moja huwa na thamani ya mtaani ya kati ya paundi 300 hadi 400 Kwa ujumla, thamani ya simu zote zilizoibwa inakadiriwa kufikia paundi milioni 20.
#airport #londonheathrowairport #airportinvestigation #northafrica #smartphones #aviationupdate #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzaniaupdates #aviationtanzanianews