Find WhatsApp Channels

Discover the best WhatsApp channels for news, entertainment, education and more. Our powerful search helps you find exactly what you're looking for.

Channels & Posts for #unitedairlines

Posts

Aviation Tanzania on Instagram: "Mhudumu wa ndege apata ulemavu wa miguu na mkono baada ya maambukizi hatari ya E. coli. Sara Dorman, mhudumu wa ndege wa muda mrefu katika shirika la ndege la United Airlines, amepata ulemavu wa ghafla baada ya kugundulika na maambukizi hatari ya bakteria aina ya E. coli. Maambukizi hayo yalimsababishia mshtuko mkubwa wa mwili (septic shock) na hali ya kiafya inayojulikana kama Hemolytic Uremic Syndrome. Hali hiyo ilimpata ghafla, na ndani ya muda mfupi maisha ya Sara yalibadilika kabisa. Akiwa bado katika majukumu yake ya kuhudumu kwenye safari za kimataifa, alipatwa na hali hiyo na kulazwa hospitalini mahututi, huku akitumbukia kwenye koma. Licha ya juhudi za madaktari na mapambano makubwa ya kiafya, madhara ya maambukizi hayo yalikuwa makubwa na yasiyoweza kurekebishwa. Madaktari walilazimika kukata miguu yake yote miwili pamoja na mkono wake wa kulia ili kuokoa maisha yake. Kutokana na hali hiyo, safari yake ya kazi katika sekta ya anga, ambayo imechukua zaidi ya miaka 25 ya maisha yake, imelazimika kukoma. Kwa sasa, Sara anakabiliwa na changamoto mpya za maisha, ikiwa ni pamoja na mazoezi ya kumsaidia kurejea katika hali ya kawaida, marekebisho ya makazi ili yaendane na hali yake ya ulemavu, pamoja na gharama kubwa za matibabu ambazo hazijafidiwa na bima ya afya. #airline #unitedairlines #flightattendant #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKkIPd-NYQv/?igsh=MWpxbTVpcjlqdTRucg== *Mhudumu wa ndege apata ulemavu ...

Aviation Tanzania on Instagram: "United Airlines Yaanzisha Safari Yake ya Sita Afrika: Washington–Dakar. Shirika la ndege la @united limeanzisha safari mpya ya moja kwa moja kutoka Washington, D.C. kwenda Dakar, Senegal. Hii ni safari ya sita barani Afrika huku safari nyingine tayari zinafanyika kutoka Washington hadi miji ya Cape Town na Johannesburg nchini Afrika Kusini, Accra nchini Ghana, Lagos nchini Nigeria, na Marrakesh nchini Morocco. Safari ya kwanza ya kuelekea Dakar, ilikuwa na jumla abiria 505, jambo linaloonesha uhitaji mkubwa wa huduma hii ya usafiri wa anga katika miji hiyo. #routeexpansion #airline #unitedairlines #africanflights #dakar #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviatamedia"

https://www.instagram.com/reel/DKUlglSsXFh/?igsh=aXpvZGwzemZ2NzF4 *United Airlines Yaanzisha Safari...

Aviation Tanzania on Instagram: "Ukichelewa kuingia ndani ya ndege dakika 45 kabla ya safari, utazuiliwa kusafiri. Shirika la ndege la United Airlines limefanya mabadiliko katika sheria ya kuwasili kwa abiria katika ndege ambapo hivi karibuni abiria wote wanaofanya safari za ndani watatakiwa kuwasili ndani ya ndege dakika 45 kabla ya safari. Awali, sheria hiyo iliruhusu abiria kuingia ndani ya ndege dakika 30 kabla ya safari, hasa kwa wale wasio na mizigo ya inayokaguliwa (checked baggage). Lakini kuanzia Juni,3, 2025, abiria wote wa safari za ndani watahitajika kuhakikisha wamekamilisha hatua ya kuingia ndani ya ndege (check-in) angalau dakika 45 kabla ya muda wa kuondoka. United Airlines imeeleza kuwa lengo la mabadiliko haya ni kuboresha utendaji kazi wa shirika, na kuwapa wafanyakazi muda wa kutosha kuwahudumia abiria kwa mambo kama vile upangaji wa viti na mahitaji mengine muhimu kabla ya safari. Shirika hilo limeeleza kuwa abiria watakaochelewa kuingia ndani ya ndege baada ya muda uliowekwa hawataruhusiwa kusafiri. Kwa abiria wanaosafiri nje ya nchi Kwa United Airlines, sheria inawataka kuingia ndani ya ndege si chini ya dakika 60 kabla ya safari. Kwa kawaida, mashirika mengi ya ndege huwashauri abiria wa safari za ndani kufika uwanja wa ndege angalau saa mbili kabla ya muda wa kuondoka, na saa tatu kwa safari za kimataifa. Lakini, baadhi ya abiria huchelewa kwa matumaini ya kuwa na nafasi ya kuingia dakika za mwisho jambo ambalo sasa halitawezekana tena kwa safari za ndani kupitia United Airlines. #airline #unitedairlines #airlinepassengers #aviationtanzania✈ #aviationtanzaniaupdates #aviata #aviataupdates"

https://www.instagram.com/p/DKM89X9MUUv/?igsh=MWpwcnJtMnlndDdkcA== *Ukichelewa kuingia ndani ya nde...

Company Name: United-intern Position: Data Science...

Company Name: United-intern Position: Data Science Intern https://main.snsgroups.com/UnitedAirlines...