Aviation Tanzania 🇹🇿
Aviation Tanzania 🇹🇿
May 31, 2025 at 02:46 PM
https://www.instagram.com/reel/DKUlglSsXFh/?igsh=aXpvZGwzemZ2NzF4 *United Airlines Yaanzisha Safari Yake ya Sita Afrika: Washington–Dakar.* Shirika la ndege la @united limeanzisha safari mpya ya moja kwa moja kutoka Washington, D.C. kwenda Dakar, Senegal. Hii ni safari ya sita barani Afrika huku safari nyingine tayari zinafanyika kutoka Washington hadi miji ya Cape Town na Johannesburg nchini Afrika Kusini, Accra nchini Ghana, Lagos nchini Nigeria, na Marrakesh nchini Morocco. Safari ya kwanza ya kuelekea Dakar, ilikuwa na jumla abiria 505, jambo linaloonesha uhitaji mkubwa wa huduma hii ya usafiri wa anga katika miji hiyo. #routeexpansion #airline #unitedairlines #africanflights #dakar #aviationtanzania#aviationtanzaniaupdates #aviatamedia

Comments